Maadhimisho ya Miaka 10 ya uanzishwaji wa MICHUZI BLOG hapa nchini, chini ya Mmiliki wake Ankal  iliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
Keki  ya maadhimisho ya miaka  1o ya MICHUZI BLOG ikiwa na keki ndogo zenye majina ya wafanyakazi wa MICHUZI MEDIA GROUP.
 Mr na Mrs Ankal  na watoto wao wakikata keki ya maadhimisho ya miaka 10 ya MICHUZI BLOG, wakishuhudiwa na baadhi ya wafanyakazi wa MICHUZI MEDIA GROUP.
Mkurugezi Mtendaji wa MICHUZI MEDIA GROUP, Ankal akilishwa keki na mkewe  katika hafra fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
 Mpiga picha wa Michuzi Blog, Avila Kakingo akifungua shampeini katika hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa MICHUZI MEDIA  
GROUP wakiwa katika picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hongera sana, Ankal Michuzi, kwa kuadhimisha kutimia kwa miaka kumi ya Michuzi Blog. Ninapozunguka Tanzania, au popote duniani, naona jinsi Michuzi Blog ilivyo sehemu ya utambulisho wa m-Mtanzania. Michuzi Blog inatuunganisha. Inachangia umoja wa Taifa.

    Ankal, binafsi nakushukuru sana kwa mchango wako katika juhudi zangu za kuendesha blogu. Nakutakia kila la heri, uendeleze libeneke.

    ReplyDelete
  2. hongera sana sikujua kama wewe ankal zefulans umeazima toka chadema. kula ccm kura chadema

    ReplyDelete
  3. Hongereni sana Ankali Michuzi na timu nzima ya Michuzi Media Group (MMG) kwa kutimiza miaka 10 sio nngwe ndogo katika kuendesha chombo Blog ya Jamii ambacho kinachangia kwa kiasi kikubwa katika kupasha habari na matukio katika jamii hiliyo afrika mashariki na nje.
    Tunawaombea Mungu chombo hiki muhimu MichuziBlog aka Blog ya Jamii kidummu milele.
    Wadau
    Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni

    ReplyDelete
  4. Michuzi na wafanya kazi ndugu na jamaa
    Hongera tena sana
    Mabrook na Mungu awazidishieni kila
    ibrahim

    ReplyDelete
  5. Ankal, Blog lilikuwa wazo poa sana, maana kupitia blog yako tumejua na tunaendelea kujua mengi huko nyumbani. You have done an exceptionally superior work of informing your follow Tanzanian on events taking place in our beloved country.
    Basi kazi hii njema na kabambe tunasihi iendelezwe tena kwa ustadi na ubunifu makini kabisa.
    Congratulations!

    ReplyDelete
  6. Imependeza! Hongera sana mkuu.....hongera sana timu nzima....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...