Familia ya Kanali Mstaafu Burchard Mushumbusi, inatoa shukrani za dhati kwa  ndugu, jamaa, marafiki na majirani wote walioshiriki nasi kwa hali na mali katika msiba wa mpendwa wetu Bi. Candida K Mushumbusi aliyefariki tarehe 24 Julai 2015 katika hospitali ya Apollo, New Delhi India na kupumzishwa katika nyumba yake ya milele tarehe 28 Julai 2015 hapa Dar es salaam.


Familia pia inatoa shukrani za dhati kwa Paroko na Mapadre wa Parokia ya Mt. Nicolaus, Kunduchi  Mtongani; Uongozi na jumuiya ya Mt. Yohane Mbatizaji Kunduchi; Mkuu wa Majeshi  ya Ulinzi ya Tanzania; Uongozi na watumishi wa Hari Singh&Sons, Benki Kuu ya Tanzania(BOT), Tanzania Food and Nutrition Centre (TFNC) , Halmashauri ya  Manispaa ya Kinondoni na VASTech.

Tunatoa pia shukrani za pekee kwa Madaktari na wauguzi wote wa hospitali za Apollo New Delhi; Ruby Hall Clinic na Inamdar za Pune; Shree Hindu Mandal, Lugalo na Regency Medical Centre;
Hatutaweza kuwataja wote kwa majina, lakini tunaomba wote mpokee shukrani zetu za dhati kwa upendo wenu kwa familia hii.

Misa ya Shukrani itafanyika siku ya Jumapili tarehe 06 Septemba 2015  katika Kanisa Katoliki la Mt. Nicolaus, Kunduchi Mtongani  saa 3:00 asubuhi.  Familia inawakaribisha wote siku hiyo kanisani na baadae saa 6:00 kwenye chakula cha mchana nyumbani kwa Kanali Mushumbusi, Kunduchi Beach.


Mungu Ailaze Roho ya Bi. Candida Mahala Pema Peponi. 
Apumzike Kwa Amani.
 AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...