Taarifa zinazosambaa kumhusu Mkuu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) Jenerali  Davis Mwamunyange zilizosambaa kwenye mitandao ya jamii kwamba amekula chakula chenye sumu na amekimbizwa jijini Nairobi nchini Kenya kwa matibabu hazina ukweli wowote.Ni uzushi.

Kwa mujibu wa taarifa za familia ya Jenerali Mwamunyange pamoja na makao makuu ya jeshi ambazo Globu ya Jamii imezisaka na kuzipata, kiongozi huyu wa JWTZ hivi sasa yupo nchini Italia kwa ziara ya kikazi ya siku tisa kama anavyoonekana pichani na hajambo kabisa na yu bukheri wa afya.

Hii ni changamoto kwa wakala wa mawasiliano nchini (TCRA) ambayo imekuwa ikilaumiwa kwa ukimya wake wa kutochukua hatua thabiti kuthibiti uongo kama huu kwa kuwatafiti, kuwabaini na kuwachukulia hatua watu kama hawa wenye nia ya kuleta taharuki na machafuko nchini.
Wananchi wengie waliohojiwa na Globu ya Jamii wanahoji endapo kama kweli TCRA ipo na kama ipo ina vifaa vya kisasa iliyodai wanavyo kuwabaini watu kama hawa, na kwa nini hawajafanya kweli toka sheria ya mitandao (Cyber Law) iliyoanza kutumika.
"Endapo kama TCRA watashindwa kumnasa mhusika wa uongo huu wa kuogofya, inabidi mamlaka husika iangalie upya ajira ya watendaji wake maana kama taasisi nyeti kama JWTZ inaguswa na wao wakae kimya tu basi ujue kuna tatizo ambalo inapaswa Serikali ilifanyie kazi", amesema msomaji mmoja wa Globu ya Jamii katika maoni yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. The mdudu, haya mara moja watafutwe au atafutwe na kupewa adhabu kali ambayo haina mfano kuna mambo yakuchezea lakini si kwa jeshi letu pendwa no way at all na nyie watu wa TCRA kama kuna watu ambao hawapo makini kwenye mambo ya usimamizi na kustop ujinga kama huu tunaomba watupishe please.

    ReplyDelete
  2. Kama yupo aseme na wananchi. wananchi wanahaki ya kuhoji pia. Huyu ni mtanzania mwenzetu na inahitajika kudhibitisha kupita shaka kwa maswali au tetesi zilizopo. Nafikiri hii itakuwa busara na siyo vita.

    ReplyDelete
  3. watanzania wanataka kusikia toka kwake, siku hizi utandawazi umekuwa kutuma video au voice ni sekunde tu

    ReplyDelete
  4. Mh tcra lazima watoe tamko na kuzibitisha kua taarifa hizo ni uongo au kweli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...