Mgombea Ubunge kwa tiketi ya
Chama Cha Mapiduzi (CCM), katika jimbo la Muheza mkoani Tanga, Balozi Adadi
Rajabu (Kulia akipokea fomu), amesema atapigana kufa na kupona kuingiza wawekezaji wilayani humo
katika nyanja ya kilimo na utalii.
Akizungumza baada ya kunadiwa na
mgombea urais wa CCM, John Pombe Magufuli, Adadi amesema mjini hapa jana kwamba
ataelekeza nguvu kubwa katika kuvutia wawekezaji ili kuiinua Muheza kiuchumi.
Magufuli, aliyemnadi Adadi kwa
kumuita “tunu ya Wanamuheza”, alisema akichaguliwa na kuungwa mkono Adadi ni mtu mwenye hazina ya uzoefu adimu na mwenye kuaminiwa na watu na
taasisi nyingi ndani na nje ya Tanzania.
Kwa safi hizo ahadi zake ni rahisi kutekelezeka na kuinua maisha ya wananchi wa Muheza..
Adadi akieleza vipaumbele vyake
na mkakati wake wa kuboresha maisha ya watu kiuchumi na kijamii, aliahidi kupigania kukuza fursa za utalii na
kuwepo kwa viwanda vya kusindika muhogo
na matunda, mazao yanayopatikana kwa wingi Muheza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...