Serikali kupitia Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imesema kuwa waangalizi wa Uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, hawatakiwi kutoa tamko lololote kuhusiana na uchaguzi au Kampeni kabla ya Tume ya taifa ya uchaguzi NEC kutangaza matokeo.
Waziri husika na Wzara hiyo, Bernard Membe amesema hayo wakati akizungumza na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania, ambapo amesema waangalizi hao wanaweza kutoa ripoti zao baada ya kuthibitishwa na Wizara hiyo au NEC na ZEC.
Amesema kuwa waangalizi wote watakuwa huru kufanya kazi zao na serikali itahakikisha wanakuwa salama kwa muda wote wakapokuwa hapa nchini, huku akiwaeleza kuwa hawataruhusiwa kufika katika baadhi ya maeneo yatakayoainishwa na Tume ya Uchaguzi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe, akijibu Maswali ya Waheshimiwa Mabalozi. Kushoto kwake ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mkuu wa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini Mhe. Juma Khalifan Mpango. Kulia kwake ni Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi, Liberata Mulamula.
Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Maharage Juma, akiwatambulisha Mabalozi waliowasili nchini hivi karibuni ambao ni mara yao ya kwanza kuhudhuria Kikao cha aina hii, Wizara ya Mambo ya Nje.
Waheshimiwa Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe, wakati wa mkutano huo uliofanyika leo 10-09-2015 katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIC) jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini Mhe.Thamsanga Dennis Mseleku akiuliza swali katika mkutano huo.
Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Filiberto Sebregondi, akiuliza swali katika mkutano huo.
Picha ya pamoja baada ya mkutano huo.
Picha zote na Reuben Mchome
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...