1.         Mwezi Machi, 2015, Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Lilipitisha  Sheria ya Kuratibu Ajira za Wageni Nchini Na.1 ya Mwaka 2015 (The Non - Citizens (Employment Regulation) Act). Sheria hii ilisainiwa na Mheshimiwa Rais mwezi Mei, 2015 na imetangazwa kuanza kutumika rasmi tangu tarehe 15/09/2015 kupitia Gazeti la Serikali Na. 406 la mwaka 2015.

2.          Sheria hii inaanzisha Mamlaka moja ya utoaji wa vibali vya ajira kwa wageni
 na Mamlaka hiyo ni Kamishna wa Kazi. 
3.            Kwa kuzingatia matakwa ya Sheria hii, Wawekezaji au Waajiri wanaokusudia kuajiri wageni nchini wanapaswa kuwasilisha maombi kwa Kamishna wa Kazi  na  hati maalum ya kibali  cha Ajira itatolewa kwa mgeni husika.
4.            Mgeni atakayepatiwa kibali cha ajira atatakiwa kuwa na kibali  cha Ukaazi ambacho kinatolewa na Idara ya Uhamiaji.
5.                      Ada ya Vibali vya Ajira italipwa kwa kuzingati aina ya daraja la kibali husika kama ifuatavyo;
                                                     i.        Daraja  A kwa Wawekezaji na waliojiajiri wenyewe-USD 1,000
                                                   ii.        Daraja B kwa Taaluma maalum zilizoainishwa chini ya Sheria-USD 500
                                                 iii.        Daraja C kwa Taaluma nyinginezo-USD 1,000
                                                 iv.        Daraja D kwa walioajiriwa na Mashirika ya Dini na ya hisani-USD 500
                                                   v.        Daraja E kwa ajili ya Wakimbizi- Bure.

Malipo au Ada  ya huduma hii italipwa  kupitia Akaunti inayotajwa hapa chini;

Name:        Permanent Secretary, Ministry of Labour and Employment
A/C No:      0250211745400
Bank:         CRDB
    Aidha ,Mfumo huu mpya wa utoaji wa vibali vya Ajira kwa wageni utaanza rasmi tarehe 1/10/2015 na maombi yawasilishwe  Ofisi ya Kamishna wa Kazi,makao Makuu ya Wizara ya Kazi na Ajira,jengo la NSSF-Mwl.Nyerere Tower,Na 42,iliyopo Barabara ya   Bibi Titi      Dar-es-salaam.

6.      Wizara inapenda kutoa Rai kwa wadau wote kutoa ushirikiano ili kutekeleza matakwa ya Sheria kwa ufanisi wa maendeleo ya nchi yetu.

Imetolewa
Ridhiwani M. wema
Msemaji.
Wizara ya Kazi na Ajira.
28/09/2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ridhiwani sasa hiki kibali kina dumu muda gani? mwaka? au miezi sita?

    ReplyDelete
  2. MWEKEZAJI TEARI ANALIPA 3050$ SASSA JUMILISHA 1000$, JOOMLE 4050$ , ALAFU UELEWE KWANINI WEKEZAJI WANAKIMBIA TANZANIA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...