Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty akitoa neno la shukrani baada ya kupokea msaada wa madawati na vifaa vya elimu kwa ajili ya shule ya msingi Mbuyuni kutoka kampuni ya Aggrey&Clifford kupitia taasisi ya Hassan Maajar Trust,wengine pichani wa kwanza kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mbuyuni Dorothy Malecela,katikati ni Afisa Mtendaji wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust Bi.Zena Tenga na kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Matangazo wa Aggrey&Clifford Bw.Oliver Mutere.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty (kushoto) akimfundisha mtoto kusoma akiwa kwenye moja ya chumba chenye madawati yaliyotolewa kwa shule ya msingi Mbuyuni na kampuni ya Aggrey&Clifford kupitia taasisi ya Hassan Maajar Trust, (kulia) ni Mkurugenzi wa Mawasiliano na Matangazo wa Aggrey&Clifford Bw.Oliver Mutere.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty (kulia) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Matangazo wa Aggrey&Clifford Bw.Oliver Mutere (kushoto) wakikata utepe kuashirikia ufunguzi wa moja ya darasa la shule ya Msingi wa Mbuyuni lililowekewa madawati mapya ambayo yametolewa kwa shule hiyo na kampuni ya Aggrey&Clifford kupitia taasisi ya Hassan Maajar Trust.
Wanafunzi wanaosoma katika shule ya awali katika shule ya msingi Mbuyuni wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kindondoni na maofisa kutoka kampuni ya Aggrey&Clifford na Taasisi ya Hassan Majaar Trust muda mfupi baada ya kumalizika hafla ya kukabidhiwa madawati.
WATOTO wa shule ya awali ya Mbuyuni iliyopo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam
wamenufaika na msaada wa madawati kutoka kwa kampuni ya Matangazo na
Mawasiliano ya Aggrey&Clifford yenye thamani ya shilingi milioni 10.Pia
kampuni hiyo imetoa vifaa mbalimbali vya kusomea kwa shule hiyo ambayo pia
inatoa elimu kwa watoto wenye ulemavu wa akili.
Msaada
huo umetolewa kupitia taasisi isiyo ya kiserikali ya Hassan Maajar Trust,nayo
ya jijini Dar es Salaam ambayo imekuwa ikijishughulisha na kuboresha mazingira
ya watoto kusomea kwa kutoa misaada ya madawati na vifaa vya kusomea mashuleni
ikiwemo vitabu na tangu ianzishwe tayari imetoa misaada kwa shule mbalimbali
nchini.
Akiongea
katika hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika shule ya msingi
Mbuyuni Meneja wa Mawasiliano na matangazo wa Aggrey&Clifford Bw.Oliver Mutere alisema kuwa msaada huo ni
kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini ambayo
inakabiliwa na changamoto mbalimbali.
“Kampuni
yetu ambayo ina mtamdao katika ukanda wa Afrika Mashariki na ikiwa imeajiri
wataalamu wa Nyanja mbalimbali inajua umuhimu wa elimu bora na ndio maana
tumetoa msaada huu kuwawezesha watoto hawa wasome katika mazingira mazuri ili
waje kuwa wataalamu wazuri katika siku zijazo na tutaendelea kuunga mkono
jitihada za kuboresha elimu nchini”.Alisema.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Taasisi Hassan Maajar Trust
ZenaTenga, alisema ana imani kuwa msaada huu utawanufaisha wanafunzi
wengi katika shule ya Mbuyuni watakaotumia madawati haya “Mazingira bora ya
kusomea ni jambo la muhimu katika kuboresha elimu nchini na huwezi kuongelea
elimu bora wakati watoto wanasoma wakiwa wamekaa sakafuni”.Alisema na kutoa
wito kwa makampuni na taasisi zingine kulivalia njuga tatizo la upungufu wa
madawati mashuleni na kulimaliza kabisa.
Kwa upande wake Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Mbuyuni Dorothy Malecela alishukuru kwa msaada huo ambaye
shule yake imepata na alitoa wito kwa wafadhili wengine kuendelea kujitokeza
kusaidia jitihada za serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali
zilizopo katika ufanikishaji wa kutoa elimu bora.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...