Hajj Sunday Manara Mkuu wa habari wa Simba
Hajj Sunday Manara Mkuu wa habari wa Simba katika ubora wake
Hajj Sunday Manara Mkuu wa habari wa Simba kama baba yake Sunday Manara 'Computer'
Rais wa Simba Mhe. Evans Aveva akitoa
maelekezo toka benchi la ufundi kama Mourinho vile...
Kwa niaba ya Rais wa klabu yenu pendwa Simba SC Mhe. Evans Aveva na uongozi mzima wa klabu napenda kuwashukuru wanachama na wapenzi wetu wote waliosafiri kutoka sehemu mbalimbali za nchi.kwenda mkoani Tanga kwa ajili ya kuishangilia klabu yenu kwenye mechi zetu za ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya timu za African sports na Mgambo
Rais na uongozi mzima wa Simba wamefarijika sana na support yenu mliyoionyesha Tanga na kupelekea kuwa na mwanzo mzuri wa ligi kwa kuzifunga timu zote mbili zinazotumia uwanja wa Mkwakwani
Pia uongozi unawashkuru sana washabiki wetu ambao hawakujaaliwa kufika Tanga kwa sala na dua zao ambazo bila shaka zilisaidia kutupa nguvu kubwa zilizofanikisha ushindi huo muhimu kwa klabu
Ni matarajio ya uongozi.support na dua zenu zitaendelea kwenye msimu mzima wa ligi hadi tutakaporejesha kombe letu.ambalo Simba ndio klabu ya kwanza nchini kulitwaa.
RECLAIMING OUR GLORY
Imetolewa na Hajj S Manara
Mkuu wa habari wa Simba
17-9-2015
Simba sports club
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...