Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akiangalia kibao cha taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyozinduliwa leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akiogea na mmoja wa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo katika taasisi hiyo
Muuguzi akiwa na mmoja wa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa moyo
Picha ya pamoja baada ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid kuizindua Taasisi hiyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam ![]() |
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akizindua Taasisi hiyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam |
Taasisi hiyo itatoa mafunzo ya Ubingwa wa juu katika fani ya Upasuaji wa Moyo , dawa ya usingizi na
Tiba ya Moyo kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi
Muhimbili( MUHAS).
Akizindua
Taasisi hiyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa
niaba ya Rais Jakaya Kikwete, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid amesema taasisi hiyo imeleta ahueni kwa wagonjwa wa moyo nchini ambapo kati ya Januari hadi Agosti
mwaka huu imehudumia wagonjwa wa nje 14, 257 ,wagonjwa waliolazwa ni 912 na
imefanya upasuaji kwa wagonjwa 148.
Kati ya wagonjwa waliofanyiwa
upasuaji ,wagonjwa watano tu ndio waliofariki Dunia ambao ni Asilimia 3. 4 ,
kiwango ambacho ni kidogo kuliko wastani uliokisiwa na wataalam wa asilimia 13.
Akifafanua amesema huduma
zilizotolewa na taasisi hiyo zimeokoa
kiasi cha Shilingi 1, 915,440,000 iwapo wagonjwa
hao wangepelekwa kutibiwa nje ya nchi.
Tuendelee kuimarisha huduma za Afya nchini kote na katika hospitali za rufaa.
ReplyDelete