Tunasikitika kuwaarifu kwamba mwenyekiti wetu wa kwanza wa mfuko Mr Michale Mgodo amepatwa na msiba wa baba yake mzazi Marehemu Godfrey Mngodo (pichani) uliotokea katika hospitali ya Dar Group jijini Dar es salaam juzi. 

Mipango ya mazishi inafanyika 
 nyumbani Tanzania na hapa USA kwa Mr and Mrs Mngodo.

Address yao ni 
549 Wildindingo Run, 
Westerville, 
Ohio 43081. 

Kwa maelezo  Zaidi please wasiliana na Michael Mngodo kwa kupitia number 614 446 5556, Teddy Mngodo 614 772 1591 na mwenyekiti wa sasa ndugu Deo Mwalujuwa kwa number yake ya 614 378 8655.
Kama kawaida yetu tunaombwa tufike 
nyumbani kwa wafiwa katika kipindi hiki kigumu cha msiba huu.
BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA.

Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha aliyekuwa mmoja wa magwiji wa Tasnia ya Utangazaji nchini Mzee Godfrey Mngodo ambaye alifariki dunia, Ijumaa, Septemba 11, 2015 mjini Dar es Salaam. 
Katika salamu zake za rambirambi kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara, Rais Kikwete amesema kuwa amesikitishwa na taarifa za kifo cha Mzee Mngodo ambaye amemweleza kama kielelezo thabiti cha weledi na ubora wa Tasnia ya Utangazaji katika Tanzania. 
“Nimesikitishwa na kifo cha Mzee Mngodo ambaye kwa kila kigezo alikuwa kielelezo thabiti cha weledi na ubora wa utangazaji katika nchi yetu. Kwa miaka mingi alichangia sana maendeleo ya nchi yetu kupitia kazi yake ya utangazaji tokea alipokuwa Redio Tanzania Dar es salaam (RTD) hadi alipohamia DTV. Tutaendelea kumkumbuka kwa mchango wake huo kwa taifa letu.” 
Rais Kikwete pia amemtaka Waziri Mukangara kumfikishia pole zake nyingi kwa familia ya Mzee Mngodo na kuwajulisha kuwa yuko nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke peponi pema roho ya Marehemu Mzee Godfrey Mngodo. Amen.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...