Mchezaji wa timu ya Ilala Rukia Annaph (kushoto)
akichuana vikali na mchezaji wa timu ya Temeke Christina Daudi katika mchezo wa
nusu fainali ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es
Salaam leo (Alhamisi September 17. Temeke ilishinda 2-1
Mchezaji wa timu ya Ilala Tumaini Michael (Kulia)
akimtoka mchezaji wa timu ya Temeke Shamimu Hamis katika mchezo wa nusu fainali
ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam leo
(Alhamisi September 17). Temeke iliibukana na ushindi wa magoli 2-1.
Mchezaji wa timu ya Ilala Jackline Albert (Kushoto)
akimtoka mchezaji wa timu ya Temeke Shamimu Hamis katika mchezo wa nusu fainali
ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam leo
(Alhamisi September 17. Temeke ilishinda 2-1.
TEMEKE
girls jana walifanikiwa kutinga hatua ya fainali, baada ya kuwagaragaza
majirani zao wa Ilala kwa kuwafunga mabao 2-1 katika muendelezo wa michuano ya
U-17 ya Airtel Rising Stars, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume jijini Dar es Salaam.
Ilala
ambao walionekana kuumiliki mpira kwa kiasi kikubwa sana katika kipindi cha
kwanza walifanikiwa kuandika bao lao mnamo dakika ya 1 baada ya Tumaini Michael
kuachia shuti na kutinga wavuni huku kipa wa Temeke akiwa hana la kufanya.
Alamanusra
Ilala wapate baola pili manmo dakika ya 20 baada ya Tumaini Michael tena kupiga
mpira wa kichwa ambao ulipaa kidogolangoni mwa Temeke.
Katika
kipindi cha pili, Temeke walionekana kucharuka huku wakicheza kwa kasi kubwa, na
ndipo mshambuliaji wa timu hiyo, Shamimu Hamisi mnamo dakika ya 40, alipomalizia
kwa umaridadi mpira uliotemwa na kipa wa Ilala na kuukwamisha moja kwa moja
wavuni na kusawazisha goli.
Temeke
waliofanikiwa kuandika goli la pili mnamo dakika ya 61 kupitia kwa Asia Juma na
kudidimiza matumaini ya Ilala kutinga hatua ya fainali.
Baada
ya mchezo huo kocha wa Ilala Omari Bwezi alisema: “Tumekubali
matokeo,wachezajiwangu walicheza vizuri kipindi cha kwanza lakini walionekana
luchoka sana kipindi cha pili na kuwapa nafasi ya kutawala wnzetu na ndio maana
tukafungwa”.
Naye
kocha wa Temeke Daudi Siang’a alisema: “Vijana wangu walifuata niliyowalekeza wakati
wa mapumziko na waliporudi uwanjani walifanya nilichowaeleza na hatimaye
tukapata matokeo”.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...