Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi akitoa utabiri wa msimu kwa miezi ya Septemba hadi Desemba 2015 kwa wanahabari.kushoto kwa Dkt, Kijazi ni mkurugenzi wa huduma za utabiri, Dkt. Hamza Kabelwa.
---------------------------------------------------------------------------------------------------
Kutokana na mwelekeo wa mifumo ya hali ya hewa iliyopo na inayotarajiwa, mvua za vuli zinatarajiwa kuwa kama ifuatavyo:
(i)     Mvua za vuli (kwa maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua)

Msimu wa mvua wa miezi ya Oktoba hadi Disemba (vuli) ni mahususi katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara), pwani ya kaskazini (Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro-kaskazini pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba), kanda ya Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga) na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma. 

Mvua zinatarajiwa kuwa za juu ya wastani hadi wastani kwa maeneo mengi. Mvua hizo zinatarajiwa kuanza mapema katika wiki mbili za mwisho za mwezi Septemba 2015 katika  kanda ya ziwa Victoria na katika maeneo machache ya Pwani ya kaskazini. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...