KAMPUNI YA RELI TANZANIA
TAARIFA  KWA VYOMBO VYA HABARI YA  KUAHIRISHA SAFARI YA TRENI KWENDA  BARA  LEO IJUMAA SEPTEMBA 11, 2015, HADI KESHO JUMAMOSI SEPTEMBA 12, 2015  SAA  11 JIONI!
  
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unasikitika kuwataarifu  abiria wote na wananchi kwa jumla  kuwa kutokana na ajali ya treni ya mizigo iliyotokea kati ya Ngerengere na Kinonko jana mkoa wa  Morogoro , safari ya  treni ya abiria kwenda Bara  iliopangwa kuondoka  leo saa 11 jioni imeahirishwa hadi kesho Jumamosi Septemba 12, 2015  saa 11 jioni.
Mafundi wa TRL wako katika eneo  la ajali tokea jana wakifanya kazi kwa lengo la  kuhakikisha njia inafunguliwa kwa wakati ili huduma ya  treni za kampuni zirejeea kama kawaida mapema hapo kesho.
Uongozi wa TRL unawaomba radhi wale wote watakaopatwa na usumbufu wowote utakaojitokeza.
Atakaye soma taarifa  hii amwarifu na mwenziwe!

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Elias Mshana
TRL Makao Makuu,
Dar es Salaam.
Septemba 11, 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...