Na John Gagarini, Chalinze 
WAZAZI wa watoto wa wafugaji kwenye Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo wametakiwa kuachana na tabia ya kuwafanya watoto wao kuwa wachungaji wa mifugo huku wakikosa haki ya kupata elimu. 
Hayo yalisemwa kwenye na Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete Mazizi kata ya Msata wakati wa mkutano wa kampeni na kusema kuwa baadhi ya wazazi wa watoto wa wafugaji wanaendeleza utamaduni wa kutowapeleka watoto wao shule na kuwaacha wakichunga mifugo ya wazazi wao. 
Ridhiwani alisema kuwa nyakati hizi siyo za kuwaacha watoto wasipate elimu kwani zimepitwa na wakati na urithi wa mtoto ni elimu na siyo mali kwani bila ya elimu mali hupotea bila ya faida yoyote kwa mtoto na familia nzima. 
“Hapa hatupaswi kuonyesha umahiri wa mtoto kuonyesha ufundi kujua anatunzwaje kikubwa ni kuwasomesha ili baadaye hata kama watakuja kuwa madaktari basi watawasaidia kuwatibia mifugo yenu kwa utaalamu,” alisema Ridhiwani. 
Alisema kuwa tamaduni kama hizo hazipaswi kupewa nafasi wakati kama huu wakati uliopo ni watoto kwenda shule ili kuwajengea maisha bora ya baadaye ambayo yatawasaidia kuliko kumnyima elimu. 
“Namshukuru Mungu pamoja na wazazi wangu kwa kunipatia elimu ambayo imenisaidia na kuweza kunifikisha hapa nilipo lakini nisingepata elimu ningekuwa wapi kwani urithi niliopewa ni elimu ambayo itanisadia katika maisha yangu yote kwani hata kama una mali huna elimu ni kazi bure lazima wazazi wabadili mitazamo na kutoa kipaumbele kwenye elimu,” alisema Ridhiwani 
 Aidha alisema kuwa moja ya vitu ambavyo anavipigania katika kipindi kijacho endapo atachaguliwa kuwa mbunge ni suala la elimu kwani anataka Jimbo hilo liwe na wasomi wengi ili waweze kuisaidia jamii ya Chalinze. 
Naye mkazi wa Msata Shaban Mtambo alisema kuwa jamii ya wafugaji bado inaona watoto kuchunga mifugo kuwa ni kazi yao jambo ambalo ni makosa kwani mtroto anakosa haki zake za msingi ikiwa ni pamoja na elimu.
 Mtambo alisema kuwa licha ya baadhi ya wazazi wa watoto wa wafugaji lakini wameendelea kuwahamasisha wazazi wenzeo kuachana na utamaduni huo ambapo wengine tayari wameshaaanza kubadilika na kuwapeleka watoto wao shule.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Msoga wakimsikiliz amgombea Ubunge Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete hayupo pichani kwenye mkutano wa kampeni.

Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kwa CCM Ridhiwani Kikwete akizungumza na wakazi wa kijiji cha Makombe kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo Almas Maskuzi kulia akimnadi mgombea wa CCM Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete kwenye Kijiji cha Pongwe Kiona.
Wakazi wa Lugoba wakimsikiliza mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete hayupo pichani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...