Na Mwandishi Wetu, Kagera 
TAASISI ya kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo, jana imewakabidhi hundi ya Sh Milioni tatu watoto watatu wilayani Biharamulo, mkoani Kagera, kwa ajili ya kunufaika na huduma ya Bima ya Elimu iliyoachwa na mzee wao Karume Ochieng aliyefariki Dunia, huku akiwa amejiunga na huduma ya bima kwa ajili ya watoto wake hao.
Mratibu Mauzo wa Bima ya Elimu wa Taasisi ya Kifedha inayotoa Mikopo(Bayport Financial Services, Ruth Bura akikabidhi mfano wa hundi kwa familia ya marehemu Karume ambaye alikuwa amejiunga na bima hiyo katika shule ya msingi Nyamuhuna iliyopo wilayani Biharamulo mkoani Kagera, kushoto ni Meneja Mauzo wa Bayport Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala. Taasisi hiyo imeanzisha bima ya elimu ili kusaidia kiasi cha ada kwa watu wa karibu walioainishwa na mteja wao endapo atakumbwa na umauti.

Watoto hao ambao wamepewa hundi hiyo itakayowawezesha kila mwaka katika vipindi vya miaka mitatu mfululizo kupewa Sh Milioni moja kwa ajili ya kuwalipia ada katika shule wanazosoma ni pamoja na Athieno Karume, Chacha Karume na Aaptalius Karume.
Makabidhiano ya hundi kwa familia ya marehemu Karume yakiendelea wilayani Biharamulo, mkoani Kagera.

Akizungumza katika makabidhiano ya hundi hiyo kwa watoto hao, Mratibu wa Bima ya Elimu ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, alisema kwamba kukabidhi hundi hiyo kutawafanya watoto hao wasome kwa raha, baada ya kuwekewa bima hiyo na marehemu baba yao kutokana na mapenzi mema na vijana hao wanaoendelea na masomo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...