
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dr. Fenella
Mkangara leo Jumapili, Septemba 13, 2015 saa 8 kamili mchana anatarajiwa
kuzindua rasmi fainali za michuano ya Airtel Rising Star katika uwanja
wa Karume jijini Dar es salaam.
Jumla ya timu sita zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo ambayo imekua
ikifanyika kila mwaka nchini kwa udhamini wa kampuni ya simu za mkononi
ya Airtel, ambapo vijana wenye vipaji huchaguliwa na kupata nafasi ya
kujiunga na vituo vya michezo (Academy) za Dakara – Senegal na Doha –
Qutar zinazomilikiwa na kampuni hiyo.
Katika
uzinduzi huo wa leo, timu za mkoa wa Ilala, Kinondoni, Mbeya, Morogoro,
Mwanza na Temeke zinatarajiwa kupambana kusaka mshindi kwa fainali hizo
za kitaifa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...