MWENYEKITI  wa Makampuni ya Quality Group Limited, Yusuph Manji (PICHANI) amenyakua tuzo ya kielelezo cha viongozi wa biashara wa Afrika kwa mwaka 2015.

Manji ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya soka ya Yanga, aliwapiku wafanyabiashara wengine wakubwa akiwemo bilionea namba moja Afrika,  Aliko Dangote.
 Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na uongozi Quality Group, ilisema  tuzo hiyo ilimshtua 'bosi' wao kwani hakutarajia na kwamba itasaidia kuvutia wawekezaji pamoja na kuongeza idadi ya watalii
nchini.  Tuzo hizo zilitolewa Septemba 16 mwaka huu.
Taarifa hiyo iliongeza ya Manji ni chachu kwa vijana kufanya vizuri kwenye sekta zao na  itasaidia nchi kusonga mbele katika kujikwamua na umasikini.  Tanzania inaendelea kujukulikana kimataifa na itasawaidia watanzania kwa ujumla kufanya kazi ama biashara katika nchi nyingine bila ya vikwazo visivyo na msingi kupitia tuzo hiyo.
Baadhi ya waliowahi kutwaa tuzo hiyo ni Mwenyekiti wa Emirates Group, Sheikh Ahmed bin Saeed Al Maktoum inayomiliki kampuni ya Ndege ya Emirates inayozidhamini timu za Real Madrid, Arsenal, AC Milan na
nyingine kubwa.
Wengine ni Mwenyekiti wa Emmar Properties, Mohammed Alabbar pia bilionea kutoka India, Ratan Tata anayemiliki kampuni kubwa yaEmeritus of Tata Sons Ltd.
Pia bilionea aliye tano bora duniani kwa utajiri, Mukesh Ambani ambaye ni mwenyekiti wa Reliance Industries Ltd. Wengine ni Yingluck Shinawatra, Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand.
Pamoja na ushindi huo wa kishindo wa Manji, pia kampuni yake ya Quality Group imeshinda kuwa kampuni bora na yenye mpangilio wa uhakika kwa bara la Afrika ikipewa tuzo ya “Most Iconic Brand 2015”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...