ZAIDI ya watu 500 wanatarajiwa kushiriki katika bonanza la
kusherehekea miaka 17 tangu kuanzishwa kituo cha mazoezi cha home gym kilichopo
mwenge jijini dar es salaa litakalofanyika juma pili hii ya septemba 20 katika
viwanja vya Escape One.
Andrew Mangomango ni mkurugenzi wa kityuo hicho
ametanabaisha kuwa maandalizi yote yamekamalika na kusema kuwa miongoni mwa
watu watakaoshiriki katika bonanza hilo ni pamoja na vikundi vya Joging vya
jijini DSM, vutio vya gym na yeyote atakayehitaji kushiriki katika bonanza hilo.
Miongonui mwa mambo yatakayoshamirisha bonanza hilo ni
pamoja na kutembelea hospitali ya palestina
ya sinza jijini DSM na kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa sanjari na
kufanya usafi katika hospitali hiyo.
Bonanza hilo litakalofanyika katika viwanja vya Escape One
litaanza Mlimani City majira ya saa kumi na mbili asubuhi kwa washiriki
kukimbia kwa mwendo wa taratibu pamoja na kutembea kwa kundi linguine.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...