KUSOMA ZAIDI kliks
goes to sheriayakub.blogspot.com
Na Bashir
Yakub
Mara kadhaa mkopaji
anaposhindwa kulipa mkopo
hukimbilia mahakamani ili
kuona kama anaweza
kupata unafuu hasa linapokuja suala
la wakopeshaji wake
kutaka kuuza nyumba/kiwanja alichoweka
rehani.
Ni ukweli
usiopingika kuwa hatua
hii imewasaidia wengi
hasa wale wanaowahi.
Yapo makala tuliwahi
kuandika kuhusu hatua za kuchukua
hasa inapotokea kuwa
nyumba yako inataka
kuuzwa.
Makala yalieleza
namna na hatua za kufuata ili
kuokoa nyumba. Kwenda
mahakamani kuzuia nyumba
isiuzwe baada ya
kushindwa kurejesha kiasi
cha rejesho sio ukorofi
isipokuwa ni kutekeleza lililo
ndani ya sheria hasa pale panapo sababu
za msingi za
kufanya hivyo.
Mahakama
za ardhi za
wilaya na mahakama
kuu hasa ya
ardhi ndizo mahakama
zenye mamlaka katika
kutoa mazuio haya
kutegemeana na thamani ya
nyumba/kiwanja na kiasi cha
deni kilichohusishwa katika
muamala huo.
Swali kwetu ni
kama baada ya
kuwa umeenda mahakamani
na kubahatika kupata
zuio la kutouzwa nyumba yako, je
upande wa wakopeshaji
wanaweza kukata rufaa kupinga
amri hiyo na kufanikiwa. Majibu ya
swali hili ndio makala
ya leo.
1.HAKI YA
RUFAA.
Kifungu cha 74 cha
sura ya 33 Sheria
mwenendo wa madai kinaeleza rufaa
katika amri mbalimbali
za mahakama. Kifungu
kilieleza wazi kuwa
kutakuwa na rufaa
kutoka mahakama za
wilaya na zile
za hakimu mkazi
ambapo rufaa hizo
zitatakiwa kwenda mahakama
kuu. Kwa wasiojua maana
ya rufaa, hii ni hatua
ya kupeleka malalamiko
mbele zaidi baada
ya kuwa hukuridhishwa
na uamuzi wa
mahakama iliyoamua shauri
lako katika hatua za
awali.
Nje ya hilo kifungu
cha 78 cha sheria hiyohiyo
kiliruhusu pia kufanyika kwa
marejeo iwapo mtu
hakuridhika na maamuzi
ya amri ya
mahakama. Marejeo ni
hatua ya mahakama
kuitisha faili tena
na kupitia kilekile
ilichoamua ili kujiridhisha
na uhalali wake. Hii
hutokea baada ya
upande wa pili
kuomba hilo kufanyika. Kwahiyo
ilikuwa ikiwezekana kutolewa
amri ya kuzuia
nyumba kuuzwa halafu
baadae faili likaitishwa
tena na kurudiwa
na kutolewa amri
nyingine ambayo inaweza
kuwa ileile ya kutouzwa au ikabadilishwa
ikawa amri mpya
ya kuuza.
2. SHERIA
YA UKOPAJI FEDHA
NA KUWEKA REHANI.
Mwaka 2008 ilikuja
sheria ambayo iliitwa
kwa jina la sheria
ya ukopaji fedha
na kuweka rehani.
Sheria hii inazungumzia
masuala yote nyeti
yanayohusu kukopeshwa fedha
na kuweka rehani
mali . Ni sheria inayoratibu
masuala yahusuyo kuuzwa
kwa mali zilizowekwa
rehani na kutouzwa kwake. Inazungumzia haki
za mkopaji na
mkopeshaji halikadhalika wajibu
wao wote katika
nafasi zao. Kutokana na ujio
wa sheria hii
masuala kadhaa katika
sheria ya ardhi
ya 1999 sambamba na sheria ya mwenendo wa
madai sura ya 33 zimelazimika
kufanyiwa marekebisho ili
kukidhi malengo kadhaa .
3. AMRI
YA KUTOUZA NYUMBA
YA MKOPO HAIKATIWI
RUFAA.
Hapo juu tuliona
kuwa awali ilikuwa
ni ruhusa kwa mtu
kukata rufaa hata
kwa amri iliyotolewa
kuzuia nyumba/kiwanja cha
mkopo kuuzwa. Mahakama
ya wilaya ingeweza
kutoa amri kuwa
nyumba fulani isiuzwe hata
kama mkopaji yuko
nje ya makubaliano
kwasababu kadha wa
kadha. Hata hivyo ilikuwa ni haki
ya mkopeshaji ambaye ndiye
hutaka kuuza nyumba
kukata rufaa na kupinga amri
hiyo.
Kama amri hiyo
ingetolewa mahakama ya
wilaya au ya hakimu
mkazi basi mkopeshaji angeweza
kukata rufaa kwenda
mahakama kuu. Na huko
ingewezekana kutolewa
uamuzi uleule au
uamuzi mpya ambapo
pengine amri ya
kutouzwa ingebatilishwa na
kuruhusu uuzaji kuendelea.
Kwa sasa kutokana
na sheria hii ya masuala ya
ukopeshaji fedha na rehani kifungu
hiki kimefanyiwa marekebisho
na sasa ni
kuwa amri ya mahakama iwe
ya wilaya au mahakama kuu
ikishapita na kutoa
zuio la kutouzwa
nyumba ya mkopaji
basi huwezi tena kukata rufaa
kupinga jambo hilo. Amri
hiyo ikishatolewa basi
inakuwa imetolewa. Ni kutokana
na hilo kichwa
cha makala haya kimekuwa , amri
ya kutouza nyumba
ya mkopo haikatiwi
rufaa.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...