Benki ya CRDB kupitia tawi lake la mjini Geita imechangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika  Shule za Msingi Mwatulole na Shule ya Msingi Geita ambayo baadhi ya majengo yalibomolewa na mvua kubwa iliyoambata na upepo mkali mwanzoni mwa mwake huu mkoani Geita. 

Sambamba na kusaidia ujenzi na ukarabati wa madarasa Benki ya crdb ilichangia maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika mjini Geita kwa sababu benki hiyo inawajali wateja wake. Maadhimisho ya wiki Huduma kwa Wateja ilianza Oktoba 5 na kumalizika Oktoba 10 ambapo Benki ya CRDB ilishiriki kikamilifu katika kazi za kijamii. Benki ya CRDB imewashuru wateja wake kupitia tawi la Geita.
Meneja wa CRDB Geita, Amini Mwakang'ata (kushoto) akimkabidhi hundi ya shilingi milioni moja Mkuu wa Shule ya Msingi Mwatulole iliyopo Mkoani Geita, Catherine Mugusi  kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mwatulole akipokea msaada wa vitabu vya ziada na kiada kutoka kwa Meneja wa CRDB Geita, Amini Mwakang'ata.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...