MARA kadhaa linapoibuka suala la kugawana mali pale ndoa inapohesabika kushindikana masuala kadhaa ya msingi na yanayohitaji uelewa huwa yanaibuka. Moja ya suala kati ya masuala ambayo huibuka ni hili la kutenganisha na kufafanua hadhi ya mali za wanandoa ili mgawanyo uweze kufanyika kwa haki. Yawezekana mwanandoa akadhani ana haki katika mali fulani lakini kumbe kisheria hana haki hiyo ni mtazamo wake ndio unamsukuma kuamini hivyo.
Halikadhalika yawezekana mwanandoa kudhani hana haki katika mali fulani kumbe anayo haki. Ili kujua una haki ipi katika mali ipi na huna haki katika mali ipi yahitajika kujua misingi ya kisheria inayotumika kugawanya mali za wanandoa.
Halikadhalika yawezekana mwanandoa kudhani hana haki katika mali fulani kumbe anayo haki. Ili kujua una haki ipi katika mali ipi na huna haki katika mali ipi yahitajika kujua misingi ya kisheria inayotumika kugawanya mali za wanandoa.
1.KUGAWANA MALI ZA WANANDOA.
Ieleweke kuwa tunapoongelea wanandoa kugawana mali tunaongelea talaka. Hakuna kugawana mali bila talaka. Na kisheria talaka inapotoka tu swali linalofuata ni habari ya mali na watoto kama wapo. Mali si lazima magari na manyumba lakini pia hata vyombo vya ndani vikiwemo vitanda, makabati, sahani n,k nazo ni mali kwa mujibu wa sheria. Navyo huhitaji mgao.
2. JE KUGAWANA MALI NI NUSU KWA NUSU ?.
Linapokuja suala la kugawana mali wengi hudhani mtindo unaotumika kugawa ni ule wa nusu kwa nusu. Jambo hili si kweli kwakuwa sheria ya ndoa 1971 iliyofanyiwa marekebisho 2002 haisemi kuwa utaratibu wa kugawana mali ni nusu kwa nusu. Sheria hii imeweka msingi mkuu wa kugawana mali ambao ndio hutumika katika mahakama zetu katika kutoa maagizo ya kugawa mali za wanandoa.
Kusoma Zaidi soma bofya HAPA AU BOFYA HAPA
Kusoma Zaidi soma bofya HAPA AU BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...