Kocha wa Simba Dylan Kerr Akimkabidhi Hamisi Kiiza Tunzo Zawadi ya Mchjezaji Bora wa Simba sport Club Mwezi September 2015
Katika kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabu ya Simba ilianzisha Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa Septemba 2015.Mshindi wa mwezi wa September, 2015 ni Hamis Kizza ambapo amepata kura 250 kati ya kura 411 zilizopigwa na mashabiki na wapenzi wa Simba na soka wa Tanzania kwa ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba News.Akikabidhiwa tunzo na kocha mkuu wa Simba Dylan Kerr, mshambuliaji wa kimataifa Hamis Kizza alisema “namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kufanikiwa kuwa mchezaji wa Kwanza kabisa kuchukua tunzo ya mchezaji bora kwa mwaka 2015, napenda kuwaahidi wapenzi na mashabiki wangu katika mchezo wa soka kuwa sasa hii ndio itakuwa chachu yangu ya kufanya vizuri zaidi nikiwa na klabu yangu ya Simba”.
Kocha Kerr alipata nafasi ya kuongea na wachezaji baada ya kugawa Tunzo na Tsh 500,000 kwa mchezaji bora ambapo alisema “Simba Nguvu Moja, wachezaji wangu huu ni wakati wa kutoa ushindani mkubwa sana kwenye mchezo wetu wa soka, viongozi wamekuja na wazo la kutoa mchezaji bora na kila mtu hapa anaouwezo wa kuwa mchezaji bora ni kwa kufanya mazoezi, nidhamu ya mchezo ukiwa uwanjani na hata nje ya uwanja na kujituma hapo unaweza kuwa mchezaji bora wa mwezi”.Akizungumza leo jijini Dar es salaam Rais wa Simba Evans Aveva alisema “Uongozi, wanachama na wapenzi wa Simba wanathamini mno mchango wa wachezaji katika kuifanya timu yetu ifanye vizuri, hivyo tumeona ni jambo la busara kuwa klabu ya kwanza Nchini Tanzania kuwa na tunzo za mchezaji wake bora. 

Tunaamini kuwa Tunzo ya Mchezaji bora wa mwezi wa Simba itaongeza ari na kujituma kwa wachezaji wetu. Sisi tukiwa kama viongozi ni kazi yetu ya msingi kuhakikisha kuwa wachezaji wetu hasa wale wanaojituma zaidi wanatambuliwa na kuenziwa’’.Akizungumza jinsi tunzo ya mchezaji bora itakavyoendeshwa, Mkurugenzi Mkuu wa EAG Group ambao ni washauri na watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba, Imani Kajula alisema “Wanachama na wapenzi wa Simba na wapenda michezo ndio watakao kuwa wanachagua mchezaji bora wa mwezi kwa kutuma jina la mchezaji wanayempendekeza kwenda kwenye namba 15460, Ni wale tu ambao wamejiunga na Simba News kupitia mtandao wa Voda na Tigo wataweza kupiga kura kuchagua mchezaji bora wa mwezi wa Simba’’
Tukumbuke kuwa unaweza kumchagua mchezaji bora wa mwezi ukiwa umejiunganisha na huduma ya Simba News kwa kutuma jina la mchezaji kwenda namba 15460. Zoezi la kumchagua mchezaji bora wa mwezi wa October, 2015 linaanza tarehe October 10, 2015. Piga kura mara nyingi zaidi kuweza kumpata mchezaji wako bora wa Mwezi October, 2015.
Simba News ni huduma iliyoanzishwa na Simba ili kuwapa wapenzi wa Simba habari mbalimbali za Simba popote pale walipo ikiwemo matokeo, majina ya wachezaji wanaocheza mechi, usajili na habari nyingine za klabu ya Simba. Kujiunga na Simba News tuma neno Simba kwenda namba 15460 ni maalum kwa Tigo na Vodacom.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...