Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwaambia wananchi wa Karatu katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Bwawani,kuwa mmoja wa viongozi wa upinzani anayempenda kwa dhati, ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt Wilbrod Slaa,amesema kuwa ni kiongozi imara asiyependa kuyumbshwa na kwamba ni kiongozi anayeweza kuwa na msimamo thabiti na mapenzi makubwa na nchi yake Tanzania.
Umati wa Washabiki na wafuasi wa CCM waliokusanyika katika uwanja wa Bwawani jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni mjini Karatu,wakishangilia  mara baada kumsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake huku akijinadi na kuomba ridhaa ya kuiongoza nchi katika kipindi cha awamu ya tano kwa nafasi ya Urais.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea Viti vya Udiwani mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Karatu jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Bwawani mjini humo mkoani Arusha.
Mgombea Uubunge jimbo la Karatu Dk.Wilbald Slaa Lorri akimuombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli pamoja na yeye mbele ya wakazi wa mji wa Karatu jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni,kulia kwake ni  Wabunge watarajiwa viti maalum wanaowakilisha wanawake mkoa wa Arusha, kushoto ni Catherine Magige na Violet Mfuko wakishangilia.  
Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli pichani kushoto akiungana na wasanii Chege na Temba kucheza muziki wakati wa  mkutano wa kampeni  mjini Karatu, mkoani Arusha.

  Mgombea urais wa Tganzania kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni mjini Mbulu, mkoani Manyara jioni ya leo
 Dkt. Magufuli akisisitiza jambo mbele ya maelfu ya wananchi wa Mbulu jijini jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwanadi wagombea ubunge na madiwani mbele ya wakazi wa mji wa Mbulu kwenye mkutano wa kampeni jioni ya leo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. CCM Songambele tunakutakia ushindi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...