Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiombewa Dua na mmoja wa kiongozi wa dini mara baada ya kusimamishwa na Wananchi wa kijiji cha Puma (hawapo pichani),alipokuwa akielekea mkoani Singida mara baada ya kumaliza mkutano wake wa hadhara wa kampeni
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimshukuru kiongozi huyo wa dini
kwa kujitolea kumuombea Dua ya heri na afya njema katika nafasi yake ya
kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia
wananchi kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani
Ikungi mkoani Singida jioni ya leo ,wakati akiwaomba wananchi hao kumpigia kura za
ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais , Wabunge na
Madiwani.
Dkt. Magufuli amesema serikali
yake itahakikisha inazisaidia taasisi mbalimbali hasa za mashirika ya
dini ambazo zinaendesha hospitali katika kupata vifaa, Ruzuku, na
ajira kwa wafanyakazi ili kuimarisha huduma za kiafya kwa jamii.
Sehemu ya umati wa Wakazi wa
mji wa Ikungi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa
kampeni,wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa
akijinadi kwenye mkutano wake wa mwisho kwa jioni ya leo,ambapo kesho
anatarajia kuendelea na kampeni mkoani Singida na baadae
kuhitimisha kampeni zake kwenye mkutano mkubwa ambao unatarajiwa
kurushwa live na kituo cha Star TV.
Kiongozi
wa Msafara wa Kampeni za Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli,Ndugu
Abdallah Bulembo akimkaribisha Mgombea Urais wa CCM Dkt.Magufuli
kuwahutubia wananchi wa Ikungi jioni ya leo na kuwaomba kumpigia kura ya
ndio ifikapo Oktoba 25 mwaka huu kwenye uchahuzi mkuu wa Urais,Wabunge
na Madiwani.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Manyoni Mashariki Ndugu Damiel Mtuka mara baada ya kukabidhiwa Kitabu cha Ilani ya chama hicho kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mapema leo mchana mjini Manyoni mkoani Singida
Wananchi wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi mkoani Singida,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli aliwahutubia na pia kuwaomba wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Singida Diana Chilolo akimpigia debe Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Mnadani Ikungi,mkoani Singida.
Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ukiwasili mjini Itigi mkoani Singida mapema leo mchana,tayari kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni mjini humo.
PICHA NA MICHUZI JR-SINGIDA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Endeleza kampeni tunahesabu siku tu.
ReplyDelete