Kutoka kulia ni Mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula 2013 Bahati Muriga , Edina Kiogwe aliyeshiriki Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 na Eva Mogeni pia alikuwa Mshiriki wa Shindano la mama Shujaa wa Chakula ambalo linaandaliwa na OXFAM Kupitia Kampeni yake ya Grow
Aliyekuwa Mshiriki wa Shidano la Mama Shujaa wa Chakula Msimu wa nne 2015 Eva Mogeni (Kushoto) akielezea kuhusu safari yao ya kwenda Addis Ababa Ethiopia kwa ajili ya  kuhudhuria mkutano wa African Rural Woman Assembly (ARWAA) na kutunga Sera juu ya kilimo na kupaza sauti za wakulima wadogo hasa wanawake ili kupata Fursa sawa katika Kilimo.
Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2014 Linaloendeshwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow Bahati Muriga(Kulia)   yenye kauli mbiu kuwa Wekeza kwa wakulima wadogo wanawake Inalipa, akielezea kwa undani juu ya Safari yake ya Kwenda Marekani pia Kushukuru Oxfam kwa kupata nafasi hiyo

WALIOKUWA washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula akiwemo Mshindi wa Shindano hilo kwa Mwaka 2014 Msimu wa tatu Bahati Muriga Wamepokea Mwaliko wa Kwenda Washington DC Marekani kuhudhuria mkutano mkuu wa Siku ya Chakula duniani unaotarajiwa kufanyika Washington DC  na Addis Ababa kwa ajili ya Kuhudhuria Mikutano Mbalimbali. Kati ya hao Bahati Muriga atakwenda Marekani na Edina  Kiogwe pamoja na Eva Mogeniw watakwenda  kuhudhuria mkutano wa African Rural Woman Assembly (ARWAA)

Eluka Kibona ambaye ni Meneja wa Utetezi wa Oxfam Tanzania alisema kuwa Bahati Muliga atahudhuria mikutano mbalimbali nchini humo inayohusu masuala ya Chakula na Kilimo wakati wa wiki zote Mbili atakazokuwa huko. Aliongeza kuwa Oxfam imethibitisha kupokea Barua ya Mwaliko wa Muriga na atahudhulia kikamilifu makongamano hayo ili apate kujifunza na kupata ujuzi ambao atautumia kwa kuwashirikisha wakulima wanawake wadogo wadogo.


 “Muriga anakwenda kuhudhuria mikutano mingi, ambayo itafanyika Washington DC na Ohio. Hii ni fursa adimu ambayo Shirika la Oxfam kupitia Oxfam Tanzania limeamua kutoa kwa kinamama hawa ili wajifunze zaidi kilimo cha kisasa na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,” alisema Eluka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...