Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kupitia mwamvuli wa Ukawa, Mhe Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mwenza wa umoja huo, Dk. Emmanuel Makaidi wakati wa ibada ya kuuaga iliyofanyika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam leo mchana. Katika ibada hiyo viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa na serikali walihudhuria.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye ibada hiyo.
Mjane wa marehemu, Dk. Emmanuel Makaidi, Modesta Ponela akiwa ameinua mikono wakati akimuaga mumewe katika ibada hiyo.
 Geneza lenye mwili wa aliyekuwa  Mwenyekiti wa chama cha National League for Democracy  (NLD) Dkt  Emmanuel John Makaidi likiwa limebebwa  kwaajili ya kuelekea makaburini mara baada ya kuagwa leo katika  viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mjane wa marehemu, Dk. Emmanuel Makaidi, Modesta Ponela akiweka mchanga katika kaburi la mumewe katika mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Sinza Dar es Salaam.

Na Dotto Mwaibale
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Profesa Mwesiga Baregu amesema kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha National League for Democratic (NLD), na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) Dk. Emmanuel Makaidi ni kiashiria tosha cha ushindi wa umoja huo.

Mwenyekiti huyo mwenza wa Ukawa, amezikwa leo jioni  katika makaburi ya Sinza jijini hapa, huku yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa Profesa Baregu aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akitoa salamu za rambirambi na kwa wanafamilia, wanandugu, wanachama na wanasiasa mbalimbali nchini walioguswa na kifo hicho wakati ibada fupi kutoa heshima za mwisho Dk.Emanuel Makaidi yaliyofanyika katika viwanja vya Karimjee.

"Tutaendelea kumkumbuka hususani pale ilipokundwa Ukawa kwani alikuwa miongoni mwa wabunge waliodiriki kususia bunge la katiba lililokuwa likiendelea," alisema.


Alisema kuwa kwa sasa nguvu ya Ukawa inaonekana kukuwa waziwazi na kifo chake kina ashiria kwamba katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika 25 mwezi huu umoja huo utashinda.

Msajili wa vyama vya siasa.
Kwa upande wake Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi alisema kifo hicho kimeacha pengo kubwa kwani alikuwa mkereketwa wa mabadiliko katika siasa.

Makamu Mwenyekiti NLD.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti NLD, Mfaume Hamisi, alisema kuwa chama hicho kitaendelea kiukumbuka na kuyasimamia misimamo na mambo aliyoyaamini Dk.Makaidi wakati wa uhai wake.

Mhe. James Mbatia.
Akizungumza kwa niaba ya Ukawa, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi na Mwenyekiti Mwenza wa umoja huo, James Mbatia alisema umoja huo utaendelea kumuenzi Dk.Makaidi na kubainisha kuwa alikuwa akiamini mageuzi na mabadiliko nchini lakini hadi leo hawako nae tena.

Msemaji wa Familia.
Kwa upande wake Oscar Makaidi ambaye ni msemaji wa familia ya marehemu aliutaka umoja huo kuendelea na kazi katika siku hizi chache zilizobaki kuelekea katika uchaguzi mkuu na kuongeza ushirikiano katika chama hicho kwani aliyekufa ni Makaidi na si chama.

Philip Mangula.
Akitoa salamu za pole na rambi rambi, Makamu Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula alitoa pole kwa wanafamilia wanasiasa kwa kuondokewa mwenzao.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...