MAMLAKA ya Chakula na Dawa nchini Tanzania, (TFDA) kwa ushirikiano na Taasisi ya TradeMark East
Africa (TMEA) imezindua mfumo wa taarifa
za kiutendaji, e-portal ambayo
itawezesha TFDA kuhudumia wateja wake
kwa mfumo wa kidigitali kwa
kutumia mtandao wa internet ambapo sasa huduma za TFDA zitatolewa moja kwa moja kupitia mtandao wa internet
hivyo kuleta ufanisi zaidi .
Mfumo unaozinduliwa leo umegharim TFDA
takriban Tsh. 300 Milion na kutoka Taasisi ya TMEA imetumia Dola za Marekani $
250,000 kwa lengo la kuboresha mfumo
huo. Uzinduzi huu unahitimisha maboresho yaliyoanza mwaka 2012. Taasisi ya TMEA imeahidi kuendelea kusaidia TFDA kuboresha
mifumo yake ya usimamizi wa huduma za
kimaabara. Msaada wa ziada utaelekezwa
kwenye kuinganisha TFDA na Tasisi za kifedha ili kuboresha mifumo ya
malipo kwa njia ya mtandao. Na hatua ya
mwisho ni TMEA itasaidia kuuingiza TFDA kwenye
mfumo wa malipo yote nchini Tanzania, kupitia dirisha moja la kitaifa (National Single Window), mradi ambao uko kwenye maandalizi.
Akizungumza
katika uzinduzi Dkt. Donan Mmbando, Katibu Mkuu Wizara ya Afya alisema,
“Mfumo huu unaozinduliwa leo utarahisisha katika kufanya maamuzi ya kiudhibiti
kwa maeneo ya utoaji wa vibali ya kuingiza bidhaa nchini na kutoa bidhaa nje ya
nchi kwa kuwa muda wa kuandaa vibali utafupishwa.
Hata hivyo mfumo huu
utasaidia katika kuhudumia wateja kwa ufasaha katika kusajili na ufuatialiaji
wa bidhaa za chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba nchini. Ubunifu huu
utasaidia kuongeza idadi ya wateja kufuata na kukidhi matakwa ya kisheria
katika udhibiti hivyo kuimarisha usalama na ubora wa bidhaa zilizopo katika
soko”
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TFDA,
Hiiti B. Sillo aliongeza,
"TFDA inaishukuru sana TMEA kwa
msaada wake kwa TFDA katika uanzishwaji wa e- portal, ambayo itarahisisha ukusanyaji wa takwimu, uchambuzi
na uhifadhi wa taarifa za usajili, uratibu na ufuatiliaji wa taarifa za vyakula, madawa,
vipodozi, vifaa tiba na kuyafuatilia maduka ya dawa nchini Tanzania. Hii itaongeza
ufanisi katika utoaji wa huduma na itarahisisha muda wa kazi na kurahisisha
kufikia maamuzi.”
Mkurugenzi wa TradeMark East Africa Tawi la Tanzania Dk Josephat Kweka aliongeza,
"Portal hii inatarajiwa kuongeza kasi ya usajili, kupunguza kwa kiasi kikubwa muda wa kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchi na muda wa
kupeleka bidhaa nje ya nchi, hivyo kuboresha
mazingira ya kufanya biashara!. TMEA
Tumefurahi kushirikiana na TFDA shirika ambalo kiungo katika kulinda na
kuboresha bidhaa za afya ya umma wa Watanzania,
huku ikihakikisha ufanisi wa viwango vya ubora na usalama wa bidhaa za vyakula, madawa, vipodozi na
vifaa tiba. "
Umuhimu wa hii e-portal ya TFDA, itawezesha wafanyabiashara kuomba na kupata vibali
vyote muhimu, kwa njia ya mtandao, bila
kulazimika kufika TFDA, na wakati huo huo,
pia utawawezesha maafisa wa TFDA,
kupitia maombi hayo, kuyakagua na kuyaidhinisha kidigitali, kwa njia ya mtandao, ambapo huduma sasa zitatolewa usiku na mchana, sasa 24 kwa siku zikiwemo Jumamosi, Jumapili
na sikukuu. (24/7) .
Huduma hizi zitaunganishwa na mtandao wa Mfumo wa Taifa wa
Malipo kupitia Dirisha Moja (National Electronic Single Window) ambao uko
kwenye maandalizi.
Mfumo huu mpya wa kidigitali unaojiendesha wenyewe,
utaboresha kasi ya utoaji wa vibali vya TFDA kuagiza, kuingiza
na kusafirisha nje ya nchi, bidhaa za vyakula, madawa, vipodozi na vifaa tiba, hivyo kuimarisha uwezeshaji wa biashara.
Portal hii imewezeshwa
na TMEA kama sehemu ya majukumu yake ya kukuza biashara ya kikanda na
ushirikiano wa kiuchumi kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
e-Portal hii ya TFDA ni mtandao unaotumia Teknolojia ya Habari na Mwasiliano (ICT)
na inajumuisha ya Mfumo wa Management
Information System (MIS) kwa watoa
huduma, na Trade Portal kwa wapokea huduma ambao ni wafanya biashara. Uwezeshaji
huu kwa TFDA, kwa msaada wa TradeMark East Africa (TMEA), unalenga kuwezesha
TFDA kuwahudumia wateja wake kwa urahisi
na kwa ufanisi zaidi.
TFDA imeanzisha Mfumo wa Usimamizi wa Taarifa za
Kiutendaji kutumika kwa ajili ya ukusanyaji wa takwimu, uhifadhi na uchambuzi wa
taarifa kuhusu usajili, kanuni na ufuatiliaji
wa vyakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na maduka ya dawa nchini Tanzania. Mfumo
huu, utaongeza ufanisi katika utoaji wa maamuz na urahisishaji kazi ya
usimamizi. Aidha, e- portal itashughulikia maombi ya leseni za kuagiza na kuuza
bidhaa kwa njia ya mtandao, (online).
Matokeo yanayotarajiwa kutokana na e-
portal hii ya TFDA ni online ni pamoja
na:
• Kuongezeka kwa ufanisi kwa njia ya kuokoa muda wa kufanya biashana na kupunguza gharama kwa kwa wadau, kufuatia kuthitajika
uwepo wa mtu wala hati katika ofisi za TFDA.
• upatikanaji wa taarifa na nyaraka kwa
urahisi kwa kuingia mara moja tuu kwenye mtandao.
• Kuongezeka kwa viwango vya ufuatiliaji.
• Kuongezeka kwa ubora wa huduma, uwazi
na uwajibikaji katika huduma zinazotolewa na TFDA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...