Mgombea urais kwa tiketi ya Tanzania
Labour Party (TLP), Maximillian Lyimo.
Mgombea urais kwa tiketi ya Tanzania Labour Party (TLP), Mhe. Maximillian Lyimo hatimaye amepiga kura yake katika Kituo cha Njia Panda, Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, baada ya mambo kuwekwa sawa. Awali Mhe. Lyimo alishindwa kupiga kura baada ya kukosekana taarifa zake kituoni hapo.
Mhe Lyimo aliyejiandikishia mkoani Dar es Salaam, jana alienda kufunga kampeni zake Jimbo la Vunjo na kulala huko. Asubuhi ya leo alienda kituo cha Njia Panda jimboni humo ili akapige kura.
Baada ya kufika kituoni hapo akiwa na kitambulisho chake cha kupigia kura, alizuiwa baada ya kukosekana fomu namba 19 ambayo kisheria inayomuwezesha mgombea urais kupiga kura ya kumchagua rais kwenye kituo chochote. Baada ya Tume ya uchaguzi kutathmini hali ilivyo na kuridhika ilimruhusu apige kura yake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...