1
Mshindi wa Shindano la Bongo Star Search 2015 (BSS), Kayumba Juma (katika), akiwa ameshikilia fedha zake muda mfupi baada ya kuibuka kidedea kwenye fainali hizo zilizokuwa zikifanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa King Solomoni uliopo Namanga jijini Dar es Salaa.
24
Baadhi ya mashabiki waliohudhuria ukumbini hapo wakifuatilia burudani hizo kwa makini.

Kayumba Juma wa jijini Dar es Salaam juzi usiku aliibuka mshindi wa shindano la kusaka vipaji vya muziki la Bongo Star Search (BSS) kwa mwaka 2015 baada ya kuwabwaga washiriki wengine watano waliofika hatua ya fainali, hivyo kutwaa kitita cha Sh50 milioni. Mbali na kuondoka na fedha hizo, kijana huyo amepewa bima ya afya ya mwaka mzima kutoka kwa kampuni ya Jubilee Insurance.

Juma aliibuka kidedea katika fainali hizo zilizofanyika katika Ukumbi wa King Solomon Hall, Kinondoni jijini Dar es Salaam zilizopambwa na wasanii mbalimbali wa muziki.

Mshindi huyo aliwabwaga washiriki wengine watano ambao walifika hatua ya fainali; Frida Amani, Nassib Fonabo, Jacqueline Kayengi, Angel Mary Kato na Kevin Gerson. Licha ya kushindwa kutwaa taji hilo washiriki hao watano walitoa ushindani mkubwa na kuwapa burudani mashabiki waliohudhuria kwenye ukumbi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera sana sana sana Mshindi wa BSS kipenzi cha wengi Kayumba Juma. Nimefurahi sana sana kwa kufanikisha ndoto zako na khatimae kuunyaka ushindi huo ambazo ndio kama mwanzo wa safari yako hiyo ya kimuziki. Natumai utaendelea kujitambuwa and be who you are and stay where you are. Usije ukalewa na sifa ama umaarufu na kujisahau ulipotoka. Binafsi ningesema mbali ya ushindi huo uliojaaliwa kuupata, pia suala zima la elimu ni muhimu kwako, khasa ukizingatia na umri wako pia ungali unaruhusu na uwezekano huo kwa sasa na khasa hapo ulipofikia sidhani kama utakuwa ni kikwazo. Nazidi kukuombea na kukutakia kila la kheri katika maisha yako ya kila siku na huko usoni wendako. Mwenyeez Mungu akulinde na kukujaaliya kila la kheri na kukuepusha na shari na mabaya yote. In Sha Allah - Ameen. Once again hongera sana sana mshindi wa BSS 2015 kipenzi cha wengi Kayumba Juma.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...