Napenda kuwajulisha Watanzania waishio Dallas, Omaha, na
Kansas City kwamba kutatolewa semina ambazo zitatoa fursa ya kujiendeleza
katika elimu ya kibiashara. Kama unatarajia kuanziasha biashara yako kwa siku
za karibuni au ndio kwanza umeanza biashara yako; basi kuna umuhimu wa kupata
mwamko/elimu zaidi juu ya uanzishaji na uendeshaji wa biashara katika viwango
vya juu.
Elimu hii ni muhimu kwa watarajiwa ili kuanzisha biashara
zenye ujasiri na ufanisi zaidi katika hatua za kupambana na upinzani wa
kibiashara, ambao kwa sasa unazidi kuwa mgumu.
1.
Ni wakati gani wa kuanzisha biashara.
2.
Ni aina gani ya biashara ya kuanziasha.
3.
Sheria zote zihusianazo na biashara.
4.
Uchaguaji wa eneo la biashara.
5.
Wateja (customer service).
6.
Ufanisi wa kibiashara (enterprise strategy).
7.
Uuzaji wa bithaa/huduma (sales and marketing).
8.
Ubora wa huduma/bithaa (total quality
management)
9.
Uendeshaji wa biashara (operations).
Jipatie seat yako kwa kujiandikisha kwenye link hii: www.tropixconsulting.com.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...