Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima (kulia), Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kutengeneza Magari ya ASHOK LEYLAND ya nchini India, Bhimasena Rau wakisaini Mkataba wa ununuzi wa magari kwa ajili ya matumizi ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambavyo ni Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI. Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima (kulia), Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kutengeneza Magari ya ASHOK LEYLAND ya nchini India, Bhimasena Rau wakipongezana baada ya kusaini Mkataba wa ununuzi wa magari kwa ajili ya matumizi ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambavyo ni Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima (katikati aliyevaa tai), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wakumi kulia), Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Jumanne Sagini (wanane kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Viongozi wa Kampuni ya Kutengeneza Magari ya ASHOK LEYLAND ya nchini India. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
SERIKALI ya Tanzania imeingia Mkataba wa ununuzi wa magari kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini na Kampuni ya Motorrama (T) LTD ambayo ni Wakala wa Magari aina ya ASHOK LEYLAND kutoka nchini India.
Mkataba huo umesaniwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Job Masima pamoja na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo ya Utengenezaji wa magari, Bhimasena Rau ukishuhudiwa na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada mkataba huo kusainiwa, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja aliishukuru Serikali kwa msaada huo ambao utasaidia kutatua tatizo la uhaba wa magari katika Jeshi la Magereza.
“Utekelezaji wa mpango huu katika Jeshi la Magereza utakuwa na manufaa makubwa kwani utapunguza tatizo la uhaba wa magari kwa ajili ya shughuli za uendeshaji na utawala pamoja na utekelezaji wa jukumu la kuwasafirisha Mahabusu kwenda mahakamani na kurudi magerezani,” alisema Minja.
Lengo kubwa la ununuzi wa Magari hayo unalenga kuboresha huduma za usafiri pamoja na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama hapa nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...