Mmoja wa wafanyakazi wa Chama Cha Albino, Christina Mbedi akielezea namna Chama cha Albino kinavyofanya kazi zake kwa Meneja wa Chapa na Mawasiliano wa Zantel, Arnold Madale wakati wa ziara ya viongozi wa Zantel ofisini kwao. Anayetizama kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Umoja wa Albino Tanzania, Ernest Kimaya.
Meneja wa Chapa na Mawasiliano wa Zantel, Arnold Madale akikabidhi msaada wa vifaa vya mawasiliano kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Chama cha Albino Tanzabua, Ernest Kimaya. Wanaotazama nyuma ni baadhi ya viongozi wa Chama cha Albino.
 Meneja wa Chapa na Mawasiliano wa Zantel, Arnold Madale akikabidhi msaada wa vifaa vya mawasiliano kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Chama cha Albino Tanzania, Ernest Kimaya. Anayetazama nyuma ni mmoja wa viongozi wa Chama cha Albino.

Viongozi wa Chama cha Albino na Zantel wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Viongozi wa Zantel kutembelea ofisi zao.

  • Yaiunganisha ofisi ya chama cha albino na huduma ya mtandao pamoja na mawasiliano ya simu
Dar es Salaam, 8/10/2015: Uongozi wa Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo umetembelea ofisi za Chama cha Maalbino Tanzania, ziara yenye lengo la kujifunza zaidi kuhusu Chama cha Maalbino kinavyofanya kazi pamoja na kuboresha ushirikiano baina yao.

Pamoja na kuzungumza na viongozi wa chama cha Maalbino, uongozi wa Zantel pia umekabidhi huduma za simu, kwa kuwapa namba maalumu pamoja na kuwaunganisha na huduma ya mtandao.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Progress Chissenga alisema huu ni mwendelezo wa ushirikiano baina ya Zantel na Chama Cha Maalbino.
Kusoma zaidi bofya HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...