Asakari polisi na wataalamu wakikagua mabaki ya chopa namba  5Y-DKK iliyoanguka jana jioni ikitokea Dar kuelekea Ludewa sehemu ya hifadhi ya wanyama ya Selous ambapo Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe, rubani Capt. William Slaa na abiria wengine wawili - Casablanca Haule na Ngondombwitu Nkwera - walipoteza maisha.
 Timu ya waokoaji wakibeba mabaki ya miili ya marehemu
 Askari wakiwa eneo la ajali 













Mbunge wa Ludewa Mhe Deogratias Haule Filikunjombe (chini) amefariki dunia katia ajali ya Chopa katika hifadhi ya wanyama ya Selous, pamoja na rubani Kepteni William Silaa (juu kulia), mfanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa na ndugu yake Marehemu Filikunjombe ambao majina  hayajapatikana mara moja.

Mhe. Deo Filikunjombe, rubani na  na abiria wengine walipata matatizo ya engine ya chopa namba  5Y-DKK jana jioni wakitokea Dar kuelekea Ludewa.

Kwa mujibu wa Meya wa Ilala aliyemaliza muda wake Mhe Jerry Silaa, ambaye ni mtoto wa rubani, hakuna mtu aliyenusurika katika ajali hiyo ya Chopa. 
"Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa rasmi kutoka kwa timu ya uokoaji kuwa imefanikiwa kufika eneo la ajali na kukuta abiria wote na rubani wamepoteza maisha.
"Ni mepoteza Baba na rubani mzuri wa nchi yetu Capt. William Silaa. Nimepoteza rafiki na kiongozi wangu Mhe. Deo Filikunjombe. Nawapa pole wote waliopoteza ndugu zao. Nawaombea marehemu mapumziko ya Amani. Nawashukuru wote walioshirikiana na familia kusaidia uokozi", amesema Mhe Jerry Silaa katika kurasa zake za mitandaoni.
tangia jana habari za kuanguka kwa nchopa hiyo zilitapakaa kila kona na katika mitandao, na kuendelea hadi leo tangia asubuhi hadi baada ya ujumbe wa Jerry Silaa kupatikana mchana huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Hoooo nakulilia Filikunjombe jembe letuuu. Mungu tuhurumie siye pamoja na nchi yetu ni nini hiki mungu, hatupumziki !!!!! RIP Deo we always remember you.

    ReplyDelete
  2. Jamani ni huzuni kubwa,pumzikeni kwa amani wote,poleni wafiwa.Ankal huyu Rubani namfananisha na Rubani Fulani alikuwa anarusha Chopa mjini Geita mwanzoni mwa miaka ya 2000 kwenye masuala ya uchimbaji madini na alijengea hoteli/"kiwanja" kimoja maarufu sana Geita Enzi hizo kinaitwa Lake View kama sikosei.Alikuwa mpole na mkarimu sana tulimpenda.


    David V

    ReplyDelete
  3. Poleni wafiwa. Mungu awatie nguvu wakati huu mnapoomboleza kwa kupotelewa na wapendwa wenu. Matumizi ya chopa nayo yapunguzwe mpaka zitakapokuwa katika hali ya usalama.

    ReplyDelete
  4. Daa inasikitisha sana

    ReplyDelete
  5. RIP na pollen wafiwa

    ReplyDelete
  6. R.I.P Mpiganaji Deo Filikunjombe

    ReplyDelete
  7. Mungu azilaze roho za Marehemu mahali pema. Jamiani hizi picha zinasikitisha. Sielewi kusoma kuwa timu ya uokoaji wakati sioni hawajajiandaa kwa hali yeyote. Mavazi, vifaa vya uokoaji na kujikinga na maambukizi yeyote. Hata machela naona kuwa ilikatwa miti ya mahali hapo. Jamani hii hali inasikitisha sana.

    ReplyDelete
  8. Kwa kweli Mungu atubariki na ccm yetu. Hii miili ililala huko huko pirini. Kweli tuko nyuma kupita kiasi. Wapumzike kwa Amani.

    ReplyDelete
  9. Wé lost a courageous guy who fought for his people.

    ReplyDelete
  10. Rip deo platun leader CCP moshi 1999/2000

    ReplyDelete
  11. Deo ni kijana ambae siku zote alisimamia na kulitetea Taifa la Tanzania kwa nguvu zake zote bila ya kujali kwamba itikadi ya chama chake kinasemaje.

    Tanzania imempoteza mtu muhimu sana; Nani atakuwepo kulitetea Taifa? Kwanini watetezi wa Taifa wanafariki sana? Nakuomba Mungu utuwekee hai watetezi waliobakia na kutuletea wengi zaidi.

    Nakuomba Mwenyezi Mungu uilaze roho ya marehemu Deo mahali pema peponi amin; Msamehe makosa na dhambi zake alizozifanya hapa duniani na huko mbinguni na siku ya mwisho nakuomba mkumbuke katika ufalme wako wa mbinguni.

    Tanzania idumu daima; Muungano udumu daima! Mungu ibariki Tanzania na watu wake.

    Asanteni.

    ReplyDelete
  12. Rest in peace Mbunge wetu, Mh. Deo Filikunjombe (Haule).

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...