Na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma .
VIJANA sita  waliokuwa  katika mafunzo ya kijeshi ya kujitolea katika kikosi cha 821 JKT Bulombora mkoani Kigoma wamefariki dunia na wengine 21 kujeruhiwa vibaya kutokana na ajali ya gari iliyotokea jioni hii.

 Mganga Mfawidhi wa hospital ya mkoa wa Kigoma Dkt. Fadhil Kibaya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo. 

 "Ni kweli leo majira ya saa moja jioni tumepokea miili minne ya vijana wa JKT ambao waliletwa hapa tayari wamefariki na majeruhi 21. "Wengine  wawili wamefariki hapa hapa wakati tukiendelea kuwapa huduma"alisema Dkt Fadhili.

 Alisema hali za majeruhi mpaka sasa siyo nzuri sana kwani wengi wameumia sehemu za kichwa na mwilini.  "Bado tunaendelea na jitahada za kuwapatia matibabu na majina ya waliopoteza maisha pamoja  majeruhi tutatoa kesho, sababu majeruhi wengi hawana fahamu"alisema. 

 Naye kamanda wa polisi mkoa wa kigoma Afande Ferdinand Mtui alisema chanzo cha ajali hiyo ni gari hilo la jeshi kushindwa kupanda mlima na kusababisha tairi mbili za nyuma kupasuka. 

 Alisema ajali hiyo imetokea katika eneo la Kasaka karibu na mizani ambapo lori  hilo la jeshi lilikuwa likitoka mjini kwenda kambini likiwa limebeba makreti ya soda na unga.
Kamati ya ulinzi na usalama ikitembelea vijana wa JKT Bulombora kikosi namba 821 ambao ni majeruhi wa ajali wakiwa wodi namba 7 katika hospital ya mkoa wa Kigoma wakiendelea kupatiwa matibabu
Baadhi ya vijana wa JKT Bulombora kikosi namba 821 ambao ni majeruhi wa ajali wakiwa wodi namba 7 katika hospital ya mkoa wa Kigoma wakiendelea kupatiwa matibabu
 Mganga mfawidhi wa hospital ya mkoa wa kigoma Dkt. Fadhil Kibaya akiongea kuhusu ajali hiyo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. poleni sana wafiwa wote na majeruhi..mwenyezi Mungu awape faraja...jamani hao majeruhi wamelazwa chini au ni macho yangu?serikali kweli inashindwa hata kununua vitanda jamani?hebu tuwe na huruma ndugu zangu..kama tumeweza kununua magari mengi makubwa ya bei kwa watendaji tunashindwaje kununua japo vitanda mahospitalini?kipi bora afya zetu au magari ya kifahari?

    Again poleni sana wafiwa na majeruhi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...