JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.

       TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
   “PRESS RELEASE” OKTOBA  30,2015.

·         WATU WATATU WANAODHANIWA KUWA MAJAMBAZI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA.


·         WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUMILIKI SILAHA KINYUME CHA SHERIA.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:
WATU WATATU WANAODHANIWA KUWA NI MAJAMBAZI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. KEFA ISRAEL MDEKWA (40) MKAZI WA MAKAMBAKO 2. EVARISTO MSEMWA (26) MKAZI WA MAKAMBAKO NA 3. KIMESHU KITIPAI (36) MKAZI WA KIJIJI CHA MODELO WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUMVAMIA MTU MMOJA AITWAYE ASHERY MPANYAKAVI (32) MKAZI WA MKONDAMI WAKIWA NA SILAHA KISU, PANGA/JAMBIA MBILI NA NONDO WAKIWA NA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.278 BMJ AINA YA TOYOTA CHASSER.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 28.10.2015 MAJIRA YA SAA 23:50 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA MKONDAMI, KATA YA MAWINDI, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, WATUHUMIWA HAO WALIMVAMIA MHANGA AKIWA AMELALA NYUMBANI KWAKE NA ALIFANIKIWA KUPIGA KELELE ZA KUOMBA MSAADA NDIPO WALIJITOKEZA WANANCHI NA KUMSAIDIA. MHANGA ALIJERUHIWA KWA KUPIGWA NONDO MDOMONI HATA HIVYO ALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA. HAKUNA MALI/KITU KILICHOCHUKULIWA KATIKA TUKIO HILO. UPELELEZI UNAENDELEA.

KATIKA TUKIO LA PILI:
WATU WAWILI WAKAZI WA CHITETE WILAYA YA MOMBA WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA SIMON BENARD (42) NA BONDIA PETER PANDISHA (38) WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA SILAHA/ BUNDUKI MBILI AINA YA GOBOLE NA BASTOLA MOJA ILIYOTENGENEZWA KIENYEJI.

WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 29.10.2015 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA CHITETE, TARAFA YA NDALAMBO, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. SILAHA HIZO ZILIPATIKANA BAADA YA KUFANYIKA UPEKUZI KATIKA NYUMBA YA BONDIA PETER PANDISHA NA KUKUTWA ZIKIWA ZIMEFICHWA KWENYE DARI LA NYUMBA. AIDHA INADAIWA KUWA, WATUHUMIWA HUZITUMIA SILAHA HIZO KUFANYA UHALIFU.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTAFUTA KIPATO KWA NJIA HALALI NA KUJIEPUSHA NA VITENDO VYA UHALIFU KWANI VINA MADHARA KWA MAISHA YAO. 

AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO ILI UPELELEZI UFANYIKE IKIWA NI PAMOJA NA KUWAKAMATA.
Imesainiwa na
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...