Taarifa zaidi kuhusu Mahujaji kutoka Tanzania waliofariki na kujeruhiwa huko Saudi Arabia


Mahujaji wengine wanane kutoka Tanzania ambao walikuwa hawaonekani tokea ajali ya kukanyagana kwa mahujaji ilipotokea Makkah nchini Saudi Arabia tarehe 24 Septemba 2015 wametambuliwa kuwa, ni miongoni mwa mahujaji waliofariki dunia.

 Kutambuliwa kwa mahujaji hao kunafanya idadi ya mahujaji wa Tanzania walipoteza maisha katika ajali hiyo kufikia ishirini (20). Majina kamili ya mahujaji hao na vikundi vilivyowasafirisha kwenda Makkah katika mabano ni Hamida Llyas Ibrahim (Khidmat Islamiya), Farida Khamis Mahinda (Ahlu Daawa), Archelaus Anatory Rutayulungwa (Khidmat Islamiya) na Said Abdulhabib Ferej (Ahlu Daawa).


Wengine ni Awadh Saleh Magram (Khidmat Islamiya), Salama Rajab Mwamba (Khidmat Islamiya), Nuru Omar Karama (Ahlu Daawa) na Saida Awaadh Ali (Ahlu Daawa).

Serikali ya Saudi Arabia inaendelea kutoa taarifa zaidi za mahujaji waliofariki dunia au kujeruhiwa katika ajali hiyo na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa itaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu wahanga wa ajali hiyo kadri itakapokuwa inazipokea.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,

Dar es Salaam

13 Oktoba, 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Poleni sana familia ya Archelaus A.Rutayulungwa japo tulifahamiana na marehemu kipindi kifupi cha hijja nilijifunza kwake mambo mengi sana kutoka kwake na jinsi alivyoipenda familia yake hata dakika chache kabla ya matatizo tuliyoyapata nilimuona akizungunza kwa simu ya baadhi na ndugu zake,it is so sad .Poleni sana lakini tumshukuru Allah kwa yote yaliotokea.Innalillah Wainailahi Rajiun

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...