|
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA
BORA
Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli
S.L.P 2643, DAR ES SALAAM
Simu: +255 22 2135747/8; 2137125;
2135222
Faksi: +255 22 2111281
Barua Pepe: chragg@chragg.go.tz
Tovuti: www.chragg.go.tz
|
Oktoba 23,
2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tamko la Tume ya Haki za Binadamu
na Utawala Bora kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria kwa ajili ya Uchaguzi Huru,
wa Haki na Amani
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imekuwa ikifuatilia kwa karibu matamshi mbalimbali
ya wanasiasa, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa Serikali, Tume ya
Uchaguzi, na Jeshi la Polisi kuhusu nini kifanyike baada ya kupiga kura siku ya
uchaguzi mkuu, Oktoba 25, 2015. Matamshi haya yamesababisha mkanganyiko na
malumbano miongoni mwa viongozi na wananchi pia.
THBUB inapenda kusema kwamba, licha ya changamoto kadhaa
zilizojitokeza katika baadhi ya maeneo, wakati wa kampeni za uchaguzi, kwa
ujumla kampeni za uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani zimefanyika nchi nzima
kwa amani na utulivu. Ni wajibu wetu sote kudumisha amani katika nchi yetu muda
wote, wakati wa uchaguzi na baada ya kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu.
Tume (THBUB) inawashukuru na kuwapongeza wananchi kwa
jinsi walivyoonyesha utulivu wakati wa mikutano mikubwa ya kampeni, ambayo
imekuwa ikivuta maelfu ya wananchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...