Wakati wananchi tukiendelea kufuatilia matokeo ya uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wa awamu ya tano, ni vema basi kujikumbusha yale ambayo yaliyofanyika katika serikali ya awamu ya nne ya Rais anayemaliza muda Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mtoto wa Msoga.
Kwa kupitia njia ya muziki bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni chini ya uongozi wake mtunzi gwiji kamanda Ras Makunja wameshusha nyimbo mbili za kumuaga Rais Jakaya Kikwete na kuyaimba baadhi ya aliyoyafanya katika awamu ya Nne.
Pata burudani kwa kusikiliza nyimbo hizi at:
Babu kubwa muziki na ujumbe mzito asanteni sana maafande wa ngoma afrika nchini na kamanda majununi ras makunja
ReplyDeleteNgoma Africa band aka ffu-ughabuni muziki mtamu lakini naona kama kawaida ya kamanda tungo zake lazima kuwe na madongo mazito ndani ,kuna mistari inasikika
ReplyDelete"Enyi mlio mbali" "enyi mlio nje" msione baridi mje JK kafanya mambo moto moto" vijembe na midongo hii anawarushia wenziwe walio ughaibuni? Kamanda ras makunja mwanamuziki mkubwa mtunzi mzuri mwenye kiwango lakini kaka midongo!
Kamanda mkuu Ras makunja kiongozi wa watoto wa mbwa wazuvendi wa Ngoma Afrika asanteni kazi nzuri sana
ReplyDeletehuu muziki sio wa kitoto kidogo milio ya mitutu ya wagagagigikoko inasikika kisindikiza ujumbe wa mkuu wao asiyefilisika mistari kamanda ras makunja
ReplyDeleteViumbe wa ajabu Ngoma Africa Band aka FFU-ughaibuni au viumbe wa ajabu anunnaki alien bin watoto wa mbwa kazi yenu tunaikubali
ReplyDeletekweli si mchezo kwata wajamaa hawa ffu,wakiamuaga kutingisha wanatingisha kweli hakuna wa kupest,hongereni sana kazi nzuri kamanda
ReplyDelete