Mheshimiwa Naibu Balozi wa Tanzania, London, Mhe. Msafiri Marwa, akizungumza machache kumkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Bwana Michael P. Mwanda, kuzungumza na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi huo. Mwenyekiti huyo wa TPDC, alipata fursa ya kutembelea Ofisi za Ubalozi mara baada ya kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Baraza la utetezi, ukuzaji na uendelezaji wa shughuli za kiuchumi (Global Local Content Council), kutokana na ugunduzi wa rasilimali za mafuta na gesi katika nchi husika, uliofanyika hapa London (13-15 October 2015), Mwenyekiti Michael Mwanda aliambatana na Mtaalam wa Mafuta na Gesi kutoka TPDC, Engineer Antelimi D nchini Uingereza.
Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Msafiri Marwa (kushoto), kwenye picha ya Pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Bwana Michael P. Mwanda (kati) na Engineer Engineer Antelimi. Ujumbe huo wa TPDC ulitembelea Ofisi hizo za Ubalozi na kupata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya Maafisa wa Ubalozi.
Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Msafiri Marwa ( wa nne, kushoto), kwenye pichani, pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Bwana Michael P. Mwanda ( wa nne, kulia) na Engineer Engineer Antelimi (pili kulia). Pichani kutoka kulia ni Bwana Magnus Ulungi (kwanza kulia), dada Isabella Kafumba, Bwana Michael Mwanda, Balozi Msafiri Marwa, Bwana Yusuf Kashangwa, Bwana Allen Kuzilwa pamoja na Kanali Jackson Mwaseba.
UJUMBE WA TPDC WATEMBELEA UBALOZI
TANZANIA ilikuwa
ni miongoni mwa nchi zilizowakilishwa kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa Baraza la
utetezi, ukuzaji na uendelezaji wa shughuli za kiuchumi (Global Local Content
Council), kutokana na ugunduzi wa rasilimali za mafuta na gesi katika nchi
husika, uliofanyika hapa London (13-15 October 2015)
Lengo kuu la
Baraza hili ni kuzifanya nchi husika zinufaike na rasilimali inayopatikana
katika nchi hizo na isiwe ni kwa wawekezaji wa kigeni tu (ambao ndio wenye
mitaji na teknolojia ya kutosha inayowawezesha kutafiti na hatimaye kufikia
kuivuna rasilimali hiyo).
Ujumbe wa
Tanzania katika Mkutano huo uliongozwa na Ndugu Michael P. Mwanda, ambaye ndiye
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC). Wajembe wengine
waliokuwa naye mkutanoni ni Engineer Antelimi D. Raphael kutoka TPDC na Yusuf
Kashangwa kutoka Ubalozi wa Tanzania hapa London.
Baada ya Mkutano
huo, ujumbe wa TPDC pia uliutembelea Ubalozi na kupata fursa ya kuongea na
watumishi juu ya masuala ya msingi yanayoihusu sekta ya mafuta na gesi nchini
Tanzania. Ndugu Mwanda alianza kwa kuieleza historia fupi ya utafiti wa mafuta
nchini, kwamba ulianza (1954) kabla hata hatujapa uhuru. Hata baada ya Uhuru,
utafutaji wa mafuta mafuta uliendelezwa tena kwa bidii zaidi hasa baada ya
kuundwa kwa TPDC. Alisema pamoja na lengo kuwa la utafutaji wa mafuta, Tanzania
haikuweza na haijaweza kuyapata, na badala yake imefanikiwa kugundua tu gesi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...