Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua application itakayowawezesha wateja wake kupata huduma zote za Airtel kwa urahisi na kupitia application ijulikanayo kama “Airtel care App”.

Application hii mpya ya “Airtel care App” ni moja kati ya huduma nyingi za kibunifu zinazotelewa na Airtel zenye lengo la kuwawezesha wateja wa Airtel kutatua matatizo yao na mahitaji yao kwa urahisi wakati wowote.

Akizungumza Wakati wa uzinduzi wa “Airtel care App” Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando alisema " Airtel tumejikita katika kutafuta, kujua mahitaji ya wateja wetu kwa lengo la kubuni bidhaa na huduma zinazokidhi na kutatua haja zao wakati wote.

“Airtel care App” inawawezesha wateja wetu, kuchagua kwa urahisi na kufanya mambo mengi zaidi katika simu zao ikiwemo kuongeza salio, kuangalia salio, kuangalia matumizi na kiasi kilichosalia, kununua vifurushi vya muda wa maongezi na intaneti, kutuma na kupokea pesa, kununua mlio wa sauti, kupata ripoti ya miamala ya pesa uliyofanya pamoja na kupata msaada kwa watoa huduma. Huduma zote hizi zinapatikana kupitia application hiyo ya “Airtel care App”bila gharama yoyote ya ziada.

Ili kupata “Airtel care App” mteja anaweza kupakua au kudownload Kupitia Google Play kwa simu aina ya Android na kwa simu Iphone wanaweza kupata huduma hii kwa kupakua au kudownload application kwenye Apple store.
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando pamoja na Afisa Masoko Intaneti wa Airtel , Eric Daniel wakionyesha huduma mpya ya Airtel Care itakayowawezesha wateja wa Airtel kudownload application na kupata huduma zote kwa urahisi kupitia simu zao .
Afisa Masoko Intaneti wa Airtel , Eric Daniel (kushoto) akionyesha kwenye simu huduma mpya ya Airtel Care itakayowawezesha wateja wa Airtel kupata kudownload application ijulikanayo kamaAirtel Care na kupata huduma zote kwa urahisi. Akishuhudia ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.
Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuzindua huduma mpya ijulikanayo kama Airtel Care itakayowawezesha wateja wa Airtel kupata huduma zote kwa urahisi mara baada ya kudownload application ya Airtel Care kwenye simu zao. Akishuhudia ni Afisa Masoko Intaneti wa Airtel , Eric Daniel.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...