Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imezindua application itakayowawezesha wateja wake kupata huduma
zote za Airtel kwa urahisi na kupitia application ijulikanayo kama
"Airtel care App"
Application hii mpya ya "Airtel care App" ni moja kati ya huduma
nyingi za kibunifu zinazotelewa na Airtel zenye lengo la kuwawezesha
wateja wa Airtel kutatua matatizo yao na mahitaji yao kwa urahisi
wakati wowote
Akizungumza Wakati wa uzinduzi wa "Airtel care App"
Meneja Uhusiano wa
Airtel, Bw Jackson Mmbando alisema " Airtel tumejikita katika
kutafuta, kujua mahitaji ya wateja wetu kwa lengo la kubuni bidhaa na
huduma zinazokidhi na kutatua haja zao wakati wote.
"Airtel care App" inawawezesha wateja wetu, kuchagua kwa urahisi na
kufanya mambo mengi zaidi katika simu zao ikiwemo kuongeza salio,
kuangalia salio, kuangalia matumizi na kiasi kilichosalia, kununua
vifurushi vya muda wa maongezi na intaneti, kutuma na kupokea pesa,
kununua mlio wa sauti, kupata ripoti ya miamala ya pesa uliyofanya
pamoja na kupata msaada kwa watoa huduma.
Huduma zote hizi
zinapatikana kupitia application hiyo ya "Airtel care App"bila gharama
yoyote ya ziada.
Ili kupata "Airtel care App" mteja anaweza kupakua au kudownload
Kupitia Google Play kwa simu aina ya Android na kwa simu Iphone
wanaweza kupata huduma hii kwa kupakua au kudownload application
kwenye Apple store.
Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari wakati wa kuzindua huduma mpya ijulikanayo kama Airtel Care itakayowawezesha wateja wa Airtel kupata huduma zote kwa urahisi mara baada ya kudownload application ya Airtel Care kwenye simu zao. Akishuhudia ni Afisa Masoko Intaneti wa Airtel , Eric Daniel
Afisa Masoko Intaneti wa Airtel , Eric Daniel (kushoto) akionyesha kwenye simu huduma mpya ya Airtel Care itakayowawezesha wateja wa Airtel kupata kudownload application ijulikanayo kamaAirtel Care na
kupata huduma zote kwa urahisi. Akishuhudia ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando
Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando pamoja na Afisa Masoko Intaneti wa Airtel , Eric Daniel wakionyesha huduma mpya ya Airtel Care itakayowawezesha wateja wa Airtel kudownload application na
kupata huduma zote kwa urahisi kupitia simu zao
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...