Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua ofa kabambe
itakayowawezesha wateja wa Airtel Money kutuma pesa kwa marafiki na
familia zao ndani ya mtandao wa Airtel Bure
Ofa hii mpya ijulikanayo kama "Okoa Mapene'' ina lengo la kuinua
huduma za kifedha na kuwapatia wateja njia rahisi ya kufanya miamala
yao ya kila siku
Akiongea wakati wa uzinduzi, Meneja Uhusiano wa Airtel Bwn Jackson
Mmbando alisema " kwa mara nyingine tena tunadhirisha kwa vitendo
dhamira yetu ya kutoa huduma za kibunifu, rahisi na zenye gharama
nafuu kupitia huduma ya Airtel Money.
Leo tunawawezesha wateja wetu
wa Airtel money nchi nzima kuokoa pesa wanapotuma pesa kwenda kwa
mtumiaji wa Airtel kwani tozo za kutuma pesa ni BURE kwa kiasi
chochote kitakachotumwa. Tunaamini ofa hii ya "Okoa Mapene'' itakuwa
kichocheo kikubwa kwa wateja kutumia huduma ya Airtel Money kwa muda
wa mienzi mitatu na zaidi"
Aliongea kwa kusema "Okoa Mapene'' ni njia mojawapo ya kuwazawadia
wateja wetu wanaotuma pesa kwa ndugu , jamaa, marafiki, familia na
washirika wao wa biashara kupitia huduma ya Airtel Money. "Okoa
Mapene'' pia kuwawezesha mawakala kupata kamisheni zaidi kutokana na
kuwa na wateja wengi watakaofanya miamala mingi kuanzia sasa.
Ili kupata kutuma pesa mteja anatakiwa kupiga *150*60# na kuunganishwa
kwenye menu ya Airtel Money na kuanza kufanya miamala yake BURE.
Hiv karibuni Airtel imewazawadia wateja wake kwa kuwapatia gawiwo la
faida watumiaji wote wa huduma ya Airtel Money na kuwawekea gawiwo
hilo moja kwa moja kwenye akaunti zao za simu.
Meneja Uhusiano wa Airtel , Jackson Mmbando akionge na waandishi wa
habari wakati wa uzinduzi wa ofa kwa wateja wake itakayowawezesha
kutuma pesa kiasi chochote cha pesa kupitia huduma ya Airtel Money
bure. Pichani ni Stephen Kimea Meneja kitengo cha Airtel Money (
kushoto) na Aliesikia Peter Afisa kitengo cha Airtel Money.
Meneja Uhusiano wa Airtel , Jackson Mmbando (katikati) pamoja na
Meneja kitengo cha Airtel Money, Stephen Kimea ( kushoto) na Afisa
kitengo cha Airtel Money, Aliesikia Peter kwa pamoja wakionyesha
kipeperushi cha ofa mpya itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma pesa
kiasi chochote cha pesa kupitia huduma ya Airtel Money bure
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...