Na Deo Kakuru, Mbeya
Ndugu Wasamaria wema na wadau,
Napenda kutumia fursa hii kukufahamisheni kuwa hatimaye dada yetu Joyce Mwambepo ametoka nyumbani yupo hospitali ya rufaa Mbeya chini ya uangalizi wa Dr. Mboma akifanyiwa mazoezi ya viungo kabla ya kuelekea hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa vipimo na matibabu.
Baada ya michango mbalimbali ambayo wasamaria wema wamekuwa wakichangia toka ndani na nje ya nchi, hatimaye Dada Joyce na mimi tutasafiri pamoja Alhamisi ijayo kwa ndege ya Fast Jet ili kwenda Muhimbili ambapo tayari mawasiliano kati ya madaktari yamekwishafanyika na atafanyiwa vipimo na upasuaji.
Hivyo tunaomba wasamaria wema na wote walioguswa kuendelea kutuunga mkono katika kipindi hiki kwa michango yao ya hali na mali ili kuhakikisha dada yetu anapona maana hana msaada wowote zaidi yetu sisi tunaojitoa kwa kile tulichojaaliwa.
Hakika michango yenu haijapotea bure.
Dada Joyce, ambaye hajainuka kitandani toka alipopata ajali mwezi Aprili mwaka jana, anawashukuru sana sana wasamaria wote waliochanga kwa ajili ya matibabu yake.
Anarishukuru pia Group la Whatsapp la WANAHABARI ambao memba wake kadhaa wamechangia na wengine kubeba dhamana ya kuratibu michango na hatimaye matibabu.
Anasema hana cha kuwalipa ila kusema ASANTE SANA SANA NA anamwombea kwa Mola awazidishie pale walipopungukiwa.
Kwa bahati mbaya mwezi April mwaka jana alipata ajali ya kugongwa na gari ambayo haikusimama kumsaidia. Ila kwa msaada wa wasamaria wema alipelekwa hospitali ya raufaa mkoani Mbeya ambako alikaa kwa miezi mitatu bila kupata matibabu.
Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwan Joyce amevunjika miguu yote miwili hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa Mbeya baada ya kukosa pesa ya kufanyia uchunguzi kwa mashine ya CT Scan na MRI kabla ya kupatiwa matibabu.
Tutaendelea kuwapa updates za kila hatua kabla na baada ya kuondoka kwenda Muhimbili kwa vipimo na matibabu.
Mawasiliano na mratibu wa msaada kwa dada Joyce
ni +255 769 512 420
Mawasiliano na mratibu wa msaada kwa dada Joyce
ni +255 769 512 420
Dada Joyce Mwambepo (27) mkazi wa Sinde jijini Mbeya akisubiri chakula kinachoandaliwa na na bibi yake mwenye umri wa miaka 80
![]() |
Mratibu wa misaada ya Dada Joyce Mwambepo, Deo Kakuru, akiwa nyumbani kwa mgonjwa Sinde jijini Mbeya na mtoto wa dada Joyce mwenye umri wa miaka 4. |
![]() |
Dada Joyce Mwambepo akiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya alikohamishiwa kwa mazoezi na maandalizi ya safari ya Dar es salaam. Chini ni miguu yake ambayo imevunjika na kupooza kiasi kwamba hawezi kukaa wala kusimama na shida zake zote anamalizia hapo kitandani kwa msaada wa bibi yake na mwanae |
Dada huyu ananitia huzuni kila nisikiapo shida zake.
ReplyDeleteBasi ndugu Deo Kakuru keep us informed of her diagnosis, prognosis na habari nyingine za maisha yake.Weka pale chini contact phone number yako utakapokuwa Dar
God bless
Kwa kweli tunaomba hiyo namba ya mawasiliano. Asante sana na Mungu awatie nguvu wote wanaomsaidia na madaktari ambao watakwenda kusimamia tiba yake.
ReplyDeletendugu Deo Kakuru pongez kwako kwakujitoa kusimamia jambo hili,Mungu akawe mponyaji kwaq dada yetu huyu.Tunakuomba pia uweze kutuwekea namba yake ya simu ili pia tuppate fursa yakuwasiliana nae katika maombezi maana tunaamini yupo Mungu muweza wa yote atakesimamia operation yake na hatimae kurejea katika hali yake ya awali.
ReplyDeleteJohn Kundi-Arusha