Na Ghalib Nassor Monero
Asalaam Alaykum Warahmatullahi wabarakatu,
Alhamdulilah....
Kwa Niaba ya wakazi wa kijiji cha Mlamleni , kitongoji cha kimbangulie , wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani ninatoa shukran za dhati kwanza Ma Admin wote wa blogs mlioshirikiana nasi katika kulitangaza jambo hili la kheri.
Pili tunawashukuru wale wote wadau ambao wameshirikiana nasi kwa hali na mali katika Ujenzi wa Jengo hili la msikiti kutoka Nyasi Mpaka kuwa katika Muonekano mpya kama mnavyo ona katika picha, Mwenyezi Mungu awalipe thawabu nyingi, awasimamie katika mambo yenu, awape rizki kunjufu za halali na kila ya kheri mnayo yatamani myapate kwa haraka. Msikiti umekwisha na tumekwisha kabidhi kwa wahusika.
Kwa sasa mahitajio yaliyobaki kama nilivyopokea kwa njia ya Risala waliyonisomea waumini wa huko wakati wa ufunguzi rasmi wa msikiti huo na ambayo pia ni Maombi kwenu:
1. Kisima cha Maji, 2.Solar power na 3.Uwezweshaji wa kununua eneo jirani na msikiti ili wapate jenga Madrasa. Na mwisho pia wanatuomba kila mazuri ambayo twaona yanafaa kwao na wao tuwasogezee.
Nikiwa kama msimamizi wa PROJECT hii , Napenda kusema kuwa tunaweza hivyo basi kuisha kwa hii Project ya kwanza ndio muendelezo wa Project No2. ambayo inakusanya:1.Msikiti, 2.Madarasa vyumba vitatu n.k, 3.Nyumba ya walimu na wanafunzi (bado kujengwa).
Tafadhali ninaomba kuleta kwenu ombi la vifaa vifuatavyo :-
1.Cement - mahitaji Mifuko 150 na kuendelea, 2.Mchanga (mahitaji loli 3 kubwa), 3.Kokoto, 4.Nondo, 5.Bati ( tunapokea kwa uwezo wa mtu ) na 6.Mbao na kila kifaa cha Ujenzi.Tunapokea kuanzia kimoja viwili na zaidi.
ACHA MATUMIZI YASIYO NA LAZIMA TENGENEZA PEPO YAKO KWA DARAJA UNAYO ITAKA HAPA DUNIANI KWA KUTOA SADAKA YENYE KUENDELEA ( Sadaqatul jaalia ) .
Kwa mawasiliano zaidi Tafadhali wasiliana , au tuma Mchango kwa Tigo pesa au Airtel Money kwa Namba zifuatazo.
+255715800772 (Whatsapp)
+255673800772
+255685800772
+255689604780 (Whatsapp)
Kwa wale walio nje ya nchi Western union & Money gram
Receiver name :- GHALIB NASSOR MONERO.
Shukran , wabilahi taufiqh
Muonekano wa Msikiti wa zamani ulivyokuwa katika kijiji cha Mlamleni katika kitongoji cha Kimbangulile wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani kabla ya kujengwa upya kwa nguvu za michango ya wasamaria wema wa ndani na nje ya nchi baada ya kuona matangazo yake kupitia blogs mbalimbali.
Muonekano wa Msikiti wa zamani ulivyokuwa katika kijiji cha Mlamleni katika kitongoji cha Kimbangulile wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani kabla ya kujengwa upya.
Muonekano wa leo wa msikiti wa kijiji cha Mlamleni katika kitongoji cha Kimbangulile wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani baada ya kujengwa upya
Maandalizi ya ufunguzi rasmi wa msikiti huo
![]() |
Muonekano wa ndani ya msikiti wa kijiji cha Mlamleni katika kitongoji cha Kimbangulile wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani baada ya kujengwa upya. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Alhamdulillah!Tunaomba ujisajili na Mpesa pia ili na sisi wengine tutumie Wave app kutuma michango.
ReplyDeleteInshaAllah tutajisajiri.
ReplyDeleteUpdates zaidi kuhusu harakati hizi pia na mengine ya kheir utazipata kupitia facebook Acount :- Kijana wa kiislam Dsm.
ReplyDelete