Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Inspekta Ibrahim Omary Samwi(kushoto), na PC Elisante Bura(kulia), wakikagua moja ya magari yanayofanya safari zake mikoani, kutekeleza mkakati wa Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani kudhibiti ajali kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka.Zoezi hili limefanyika muda mfupi kabla ya magari kuondoka katika kituo Kikuu cha mabasi Ubungo,jijini Dar es Salaam kuelekea mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Inspekta Ibrahim Omary Swami(aliyeko chini ya uvungu wa gari), akikagua moja ya magari yanayojiandaa kuelekea mikoani, zoezi ambalo limefanyika muda mfupi kabla ya magari kuanza kuondoka katika kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam.aliyenyoosha kidole juu ni PC Elisante Bura. Hatua hii ya Jeshi la Polisi nchini linalenga kudhibiti ajali kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka.
Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Sajenti Jackson Mafuru (kulia), na PC Elisante Bura(kushoto), wakikagua moja ya magari yanayofanya safari zake mikoani. zoezi hili ambalo limefanyika muda mfupi kabla ya magari kuondoka katika kituo Kikuu cha mabasi Ubungo,jijini Dar es Salaam, ni moja ya hatua ya Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani kudhibiti ajali kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...