Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohamed Mpinga, akisalimiana na Mabalozi wa Usalama Barabarani, muda mfupi kabla ya kuzindua Operesheni ijulikanayo kwa jina la “Paza Sauti” yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga, akitoa maelekezo ndani ya moja ya basi linalofanya safari zake mkoani wakati wa kuzindua wa Operesheni Paza Sauti yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
Wadau wanaotumia usafiri wa barabara, wakiwemo madereva na abiria wakimsikiliza Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga(hayupo pichani) alipozindua Operesheni Paza Sauti, yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani,Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo na Matukio wa Mabalozi wa Usalama Barabarani,Jackson Kalikumtima(kulia), akitoa elimu kuhusiana na Operesheni ya Paza Sauti kwa mmoja wa wadau wanaotumia usafiri wa barabara, Operesheni hii ilizinduliwa Stendi ya Mabasi yaendayo mikoani ya Ubungo, jijini Dar es Salaam leo.(Picha zote na Abubakari Akida,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...