Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Golden Fleet LTD na Golden Coach LTD Bw. Mohamed Raza Dewji (kulia) akimkabidhi Afisa Uuguzi wa Idara ya Uuguzi na Ubora wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Bi. Mariana Makanda msaada wa vitanda thelasini na magodoro thelasini, katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja wa hospitali hiyo Bw. Aminiel Eligaesha.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Golden Fleet LTD na Golden Coach LTD Bw. Mohamed Raza Dewji (kulia) akieleza kwa waandishi wa habari jinsi alivyoguswa na tatizo la wagonjwa kulala chini mara baada ya Rais John Magufuli alipotembea hospitali hiyo.
 Daktari akimpatia huduma mgonjwa kwa kutumia mashine ya MRI ambayo ilikuwa mbovu kwa muda mrefu ila imetengamaa mara baada ya Rais John Magufuli kufanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuagiza matengenezo ya haraka yafanyike. 
 Madaktari wakifuatilia kwa makini jinsi mashine ya MRI inavyofanyakazi mapema hii leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Picha zote na Eliphace Marwa - MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Napiga vigelegele
    Tunawangojea matajiri wengine wajitokeze kwa mjengo mpya wa nchi.

    ReplyDelete
  2. Ila lengo lisiwe kusamehewa kodi au kupewa ruzuku.

    ReplyDelete
  3. Pesa za vitanda na magodoro tunazo tunachotaka ni watu kama kina Dewji walipe kodi #Hapanikazitu. Tumeshanyoywa na kunyanyasika vya kutosha na haya mafisadi

    ReplyDelete
  4. He he makubwa haya mlikua wapi b4 mpaka mjitokeze hii Leo? Hatutaki watu wanafki vigodoro 30 ndio nini sasa? tulieni acheni papara kila fisadi tutamgusa hii ni new Tanzania chini ya MAGUFULI mmekwisha na mtatia akili hakuna tena msamaha wa kodi wala ruzuku kama kweli mmeguswa na hali ilivyo hapo Muhimbili kwakua nyinyi ni matajili wakubwa tunataka kuona mnaenda na Mashine mpya kabisa kama 20 hivi coz tatizo halipo Muhimbili tu ni Tanzania nzima kuanzia sasa tunataka kuona matajili wote ndani ya Tanzania yetu wana wasaidia watanzania kwenye mambo muhimu kama vile kujenga mashule ya kisasa, mahosipital ya kisasa, upatikanaji wa maji safi na mengineyo mwisho wa kutesa kivyenu vyenu umefika kama hutaki kushea anza mapema enough is enough

    ReplyDelete
  5. Hapa kazi tu. Sio raisi kaonekana mahali furani nanyi pia vihehele wa kupeleka vijimisaada mbuzi ili jumuiya iwaone, mwendo ni mdundo tu wa kulipa kodi, kodi ndio itanunua magodoro mengi sio 30. Initiativet, toa tu usitegemee msamaha wa kodi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...