Sehemu ya mizinga hiyo iliyokabidhiwa.
Afisa Utumishi, Allan Mwela akikabidhi moja ya mizinga kwa mwanachama wa kikundi cha wafuga nyuki kutoka kijiji cha Utosi kilichoko wilaya ya Mufindi 
Baadhi ya wafugaji nyuki wakisikiliza hotuba ya mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela. (picha na Denis Mlowe.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesera akizungumza na wafugaji mara baada ya kukabidhi mizinga ya nyuki.
Mkuu wa wilaya Richard Kasesela akikabidhi moja ya mizinga 175 kwa mfugaji nyuki kutoka Kiwele.( PICHA NA NA DENIS MLOWE, MUFINDI).


NA DENIS MLOWE, MUFINDI

TIMU ya Wanasheria Watetezi wa Mazingira kwa Vitendo (LEAT) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) umetoa jumla ya mizinga ya kufugia nyuki 350, kwa vikundi 16 vya wilaya ya Mufindi na Iringa vilivyoko katika mkoa wa Iringa.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa mizinga hiyo iliyofanyika katika kata ya Sadan wilayani Mufindi juzi, Afisa mradi wa LEAT kutoka Mufindi Jamal Juma alisema lengo la mradi huo ni kuimarisha uhifadhi wa mazingira na kuongeza kipato cha jamii kwa njia ya kufuga nyuki na kupanda miti.

Alisema kuwa malengo mengine mahususi ya mradi huo ni kuleta ufanisi wa kulinda, kutunza na kutumia kwa njia endelevu rasilimali za misitu na kuongeza kipato cha mwananchi mjasiriamali mara baada ya mauzo ya asali iliyovunwa kupitia mizinga hiyo.Alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache yenye utajiri mkubwa wa rasilimali za asili mathalani misitu na wanyapori hivyo kuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Juma alisema kuwa kutokana na hali hiyo kuna changamoto mbalimbali za usimamizi na uhifadhi zikiambatana na uchomaji moto ovyo, kuchoma mkaa,ukataji miti uliokithiri na ujangiri mambo ambayo inasababisha hasara kwa taifa.Alisema kuwa kutokana na changamoto hizo husababisha umaskini, kukauka kwa vyanzo vya maji kutoweka kwa uoto wa asili na kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabia nchi.

“ Mradi huu utasaidia sana jamii ya watu wa wilaya ya Mufindi walioko katika vikundi vya ufugaji nyuki kuhakikisha unaboresha kipato kwa kuendesha mafunzo ya ufugaji nyuki na uvunaji, upandaji miti,kusaidia jamii kwa kuzipatia vitendea kazi vya ufugaji nyuki kama hivi ambavyo leat imetoa kwa kusaidiana na USAID utasaidia kuondokana na changamoto zote hizo endapo utafanyiwa kazi kwa umakini. “ alisema

Alisema kuwa awamu ya kwanza ya mradi vimenufaisha vikundi 8 vyenye watu 22 vilivyoko katika vijiji vya Lugoda, Lutali, Igombalavanu, Uhimbila, Mapogoro, Utosi, Tambalang’ombe, Kibada na Nyololo katika wilaya ya Mufindi na vikundi 8 katika wilaya ya Iringa ambapo kila kikundi kimepata mizinga 22 kama mtaji .

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mufundi,Joika Kasunga katika hotuba yake iliyosomwa na Afisa Utumishi, Allan Mwela amewaasa wananchi wanaokaa pembezoni mwa misitu kuacha kufanya shughuli za uhalibifu wa msitu ikiwemo uchomaji moto kwa ajili ya uwindaji shughuli za kilimo pamoja na uchomaji wa mkaa.

Aidha amewataka wananchi wa kuitunza vizuri misitu ili kuweza kuendelea kupata mvua kwa wingi na kuondokana na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyopo kwa sasa kwani misitu inavyoathiliwa na wananchi kwa matumizi ya kila siku na kusema kuwa chanzo cha misitu hiyo kuharibika ni kutokana na wananchi wenyewe.

“Uhifadhi wa misitu sio suala la mtu mmoja au kundi moja ila la watu wote hii inatokana na ukweli kwamba madhara yatokanayo na uaribifu wa mazingira hayana mipaka na humpata kila mtu hivyo ni wajibu wa kila mtanzania kushiriki katika kulinda maliasili” alisema .

Aliwapongeza Leat kwa kuweza kuwasadia wajasiliamali walioko katika vikundi vya kuondokana na umaskini kwa njia ya ufugaji wa nyuki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...