Na Bashir Yakub
Kesi/shauri lolote
iwe jinai au
madai kuishinda kwake
mara nyingi hutegemea
mambo makuu mawili. Kwanza mashahidi ,pili ushahidi. Mashahidi siku
zote ni watu.
Hakuna kitu kinaweza
kuitwa mashahidi halafu
kisiwe binadamu.
Hii ni tofauti
na ushahidi. Ushahidi si
lazima wawe binadamu.
Vitu hasa vizibiti(exhibit) ndivyo
huitwa ushahidi. Nyaraka,
mali, vifaa, na
kila kitu ambacho
mtu anaweza kukitumia mahakamani kuthibitisha kile
anachokisema huitwa ushahidi.
Yumkini
yawezekana wakati huohuo
mmoja ukawa na
vyote yaani ushahidi
pamoja na mashahidi hapohapo.
Hii hutegemea namna mtu alivyojiandaa
katika kuwasilisha kesi
yake.
1.SIFA ZA SHAHIDI.
Si kila mtu
ana sifa za
kuwa shahidi. Shahidi hutakiwa
kuwa mtu mkweli , muaminifu na
muadilifu. Lakini pia
sifa kuu ya
shahidi ni kuwa
na akili timamu.
Mtu asiye na
akili timamu hawezi
kuwa shahidi. Lakini pia
mtu mwenye sifa
ya uongo hasa
huko nyuma kama
aliwahi kutoa ushahidi
wa uongo mahakamani
na ikathibitishwa kuwa
alitoa ushahidi wa
uongo basi naye
hupoteza sifa ya
kuwa shahidi.
Pia sifa nyingine
kuu ya shahidi
ni muhimu awe
ni yule aliyeona,
kuhisi kwa kutumia
moja kati ya
viungo vyake, au
kusikia . Hii ina
maana shahidi hutakiwa kuwa yule anayelijua
tukio kwa kulishuhudia
na si vinginevyo
2.
IDADI YA MASHAHIDI
INAYORUHUSIWA.
Hakuna idadi
ya mashahidi rasmi
inayoruhusiwa kisheria. Idadi
yoyote ya mashahidi inaruhusiwa.
Suala la msingi
hapa ni kuwa
kila shahidi katika
mashahidi hao unaowaleta
awe na umuhimu
katika kesi. Usilete
watu ambao hawahusiki
na kuisababishia usumbufu
mahakama. Hii ni kwasababu
wingi wa mashahidi hauakisi ushindi
katika kesi. Hata shahidi mmoja
tu kama ni
wa muhimu anaweza kukufanya
ushinde kesi na kumshinda mwenye
mashahidi ishirini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...