Na Bashir Yakub.
Ardhi inaweza kumilikiwa na mtu zaidi ya mmoja. Inaweza kuwa nyumba au kiwanja. Vyote hivi vinaweza kumilikiwa na mtu zaidi ya mmoja. Kumiliki ardhi kwa zaidi ya mtu mmoja sio lazima iwe kwa wanandoa. Inaweza kuwa ndugu , marafiki , kikundi cha watu kama wafanyabiashara, wana saccos, kikundi cha michezo na aina yoyote ya kikundi cha kimaendeleo. Umiliki wa ardhi kwa pamoja unatofauti na umiliki binafsi yaani umiliki wa mtu mmoja mmoja. Tutaona tofauti hizo na mambo mengine ya msingi kuhusu umiliki wa pamoja.
1.AINA ZA UMILIKI ARDHI.
Kwa kuangalia ardhi katika mrengo wa umiliki tunaweza kusema kuwa ardhi humilikiwa kwa namna mbili. Kwanza umiliki wa mtu mmoja mmoja na pili umiliki wa pamoja. Huu ni ule niliosema kuwa ni mtu zaidi ya mmoja.
Umiliki binafsi wa ardhi yaani umiliki wa mtu mmoja mmoja unatoa haki kwa mmiliki huyo kuitumia ardhi bila kuhitaji ridhaa ya mtu mwingine yoyote. Anaweza kuuza, kuweka rehani kama dhamana ya mkopo, kutoa zawadi, kupangisha na matumizi mengine yoyote halali. Atafanya yote haya bila kuhitaji ridhaa ya mtu mwingine yoyote.
Hii ni tofauti na umiliki wa ardhi wa pamoja. Katika umiliki wa aina hii mtu mmoja hawezi kuuza, kutoa zawadi, kuweka rehani kupangisha au kuruhusu matumizi ya ardhi kwa namna yoyote ile bila ridhaa ya wengine. Kama ni wawili basi ridhaa itabidi itokane na wawili lakini pia kama ni kumi, saba , watano au zaidi basi ridhaa yao wote itatakiwa kabla ya kufanyika kwa muamala wowote ule.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...